Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Italia Yaahidi Kuwekeza Katika Hifadhi ya Mazingira

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Azzan Zungu akisalimiana na Balozi wa Italia nchini Tanzania Mhe. Roberto Mengoni mara baada ya kuwasili katika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais, Mtaa wa Luthuli Dar es Salaam. Mazungumzo baina yao yamejikita katika nyanja za kuhifadhi na kusimamia mazingira nchini.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Zungu amesema Serikali ya Tanzania iko tayari kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Italia katika nyanja za Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira.

Hayo ameyasema hii leo Jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia hapa nchini Mhe. Roberto Mengoni katika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Azzan Zungu pamoja na Balozi wa Italia nchini Tanzania Mhe. Roberto Mengoni wakiwa katika kikao cha pamoja, (katikati) ni Bi. Haikael Shishira na Kisa Mwaseba maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Bi. Kemilembe Mutasa, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira.

Amesema suala la Mabadiliko ya Tabianchi ni changamoto kubwa duniani kwa hivi sasa na nchi zinazoendelea ndio waathirika wakubwa kutokana na uchafuzi wa mazingira unaofanywa na nchi zilizoendelea.

Waziri Zungu ametoa wito kwa Serikali ya Italia kuendeleza mashirikiano katika nyanja za udhibiti wa taka na kujenga uwezo katika uzalishaji wa nishati mbadala ili kukabiliana na uharibufu wa mazingira unaotokana na ukataji wa miti kwa matumizi ya kuni na Mkaa.

“Serikali ya Rais John Joseph Pombe Magufuli inatekeleza ujenzi wa mradi mkubwa wa kufua Umeme katika maporomoko ya Mto Rufiji kwa lengo la kuongeza nishati ya Umeme na kukuza sekta ya viwanda nchini” Zungu alisisitiza.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Azzan Zungu akizungumza na Balozi wa Italia nchini Tanzania Mhe. Roberto Mengoni katika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais Luthuli Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine, nchi hizi mbili zimekubaliana mikakati ya pamoja ya kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya Tabianchi.

Asema kukamilika kwa mradi wa kufua umeme wa Mwalimu Julius Nyerere utachochea jitihada za Serikali za kupambana na uharibifu wa mazingira utokanao na ukataji wa miti kwa matumizi ya nishati ya kupikia. Ameongeza kusema kuwa jitahada za dhati zinatakiwa kuwepo pia katika uzalishaji wa umeme wa nishati ya jua na upepo.

Kwa upande wake Balozi wa Italia nchini Tanzania amesema kuwa nchi yake inalenga kutoa msukumo zaidi katika mapambano dhidi ya athari za mabadiliko ya Tabianchi, kuhimiza kilimo rafiki kwa mazingira, nishati mbadala na nishati jadidifu.

Waziri Zungu amemuhakikishia Balozi Roberto ushirikiano wa dhati katika kupambana na uharibufu wa mazingira nchini ili kuhakikisha Tanzania inabaki salama kwa taifa la sasa na vizazi vijavyo.

Italia Yaahidi Kuwekeza Katika Hifadhi ya Mazingira

11 thoughts on “Italia Yaahidi Kuwekeza Katika Hifadhi ya Mazingira

 • Pingback: sildenafil

 • August 11, 2020 at 2:08 pm
  Permalink

  It is the best time to make some plans for the long run and it is time to be happy.
  I have read this put up and if I may I want to counsel you some fascinating things or suggestions.

  Perhaps you can write subsequent articles relating to this article.

  I want to read even more things about it!

  Reply
 • August 25, 2020 at 3:17 am
  Permalink

  If you would like to increase your experience just keep visiting this web site and be
  updated with the most recent gossip posted here. 31muvXS cheap flights

  Reply
 • August 25, 2020 at 5:35 pm
  Permalink

  This site was… how do you say it? Relevant!!
  Finally I have found something which helped me. Thank you!

  Reply
 • August 27, 2020 at 10:53 pm
  Permalink

  Thanks a bunch for sharing this with all of us you
  actually understand what you’re talking about! Bookmarked.

  Please additionally consult with my site =).

  We will have a link exchange agreement among us

  Reply
 • August 31, 2020 at 5:06 am
  Permalink

  Good web site you have got here.. It’s difficult to find high-quality writing like yours nowadays.
  I seriously appreciate individuals like you! Take
  care!!

  Reply
 • August 31, 2020 at 4:31 pm
  Permalink

  Hello, Neat post. There is an issue with your website in internet explorer, may
  check this? IE still is the market chief and a huge part
  of people will leave out your wonderful writing due to this problem.

  Reply
 • June 21, 2021 at 6:51 am
  Permalink

  Outstanding story there. What occurred after?
  Take care!

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama