Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Aprili 20, 2026 ametimiza ahadi yake kwa kumkabidhi kitimwendo Helena Joseph Mwandu, mwenye mahitaji maalum, katika ofisi yake ya Mlimwa jijini Dodoma.

Ahadi hiyo ilitolewa Aprili 19, 2026 baada ya Waziri Mkuu kufanya mazungumzo na Helena kufuatia mkutano wa hadhara aliouhutubia katika Uwanja wa Shule ya Msingi Msanga, wilayani Chamwino, Dodoma.
Akizungumza baada ya kupokea kitimwendo hicho, Helena amemshukuru Waziri Mkuu kwa msaada huo, akieleza kuwa utarahisisha kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa shughuli zake za kila siku.

Hatua hiyo inaonesha dhamira ya Serikali ya kuendelea kuwajali na kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum ili kuboresha maisha yao na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii na kiuchumi.