Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Lugha ya Kiswahili ni Daraja la Mawasiliano na Utambulisho wa Taifa
Apr 08, 2026
Lugha ya Kiswahili ni Daraja la Mawasiliano na Utambulisho wa Taifa
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Riziki Pembe akifungua Kongamano la 16 la Chama cha Wanafunzi na Wahitimu wa Kiswahili wa Vyuo Vikuu na vya Kati Tanzania((CHAWAKITA), leo Aprili 08, 2026, jijini Dodoma.
Na Mwandishi Wetu

MHE. RIZIKI PEMBE: LUGHA YA KISWAHILI NI DARAJA LA MAWASILIANO NA UTAMBULISHO WA TAIFA

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Riziki Pembe amesisitiza umuhimu wa Lugha ya Kiswahili kama chombo kikuu cha mawasiliano na utambulisho wa Taifa, akieleza kuwa Kiswahili si lugha ya maneno matupu tu bali ni nyumba ya fikra, kioo cha utambulisho, daraja la mawasiliano na hazina ya historia yetu.

Ameyasema hayo leo Aprili 08, 2026 wakati alipofungua Kongamano la 16 la Chama cha Wanafunzi na Wahitimu wa Kiswahili wa Vyuo Vikuu na vya Kati Tanzania((CHAWAKITA) jijini Dodoma akishadadia kuwa lugha ndio nguo ya fikra inapohifadhiwa hulinda pia utambulisho wa watu wake.

Aidha, Mhe. Riziki ameongezea kwa kusema kuwa Kiswahili si tu ni lugha ya mawasiliano bali pia ni lugha ya kiuchumi, diplomasia, na utambulisho wa Mwafrika.


Vilevile, amewataka Wanafunzi na Wahitimu wa Lugha hiyo kuangazia ni kwa namna gani Kiswahili kinaweza kunufaika na Mapinduzi ya nne ya viwanda, Lugha hiyo ikistawi katika mifumo ya akili unde, Tafsiri za sheria, na katika Vyombo vya habari vya kidigitali hii ni kutokana na ukweli kwamba dunia ya leo inaendeshwa na kasi ya Sayansi na Teknolojia

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi