Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Fedha Sherehe za Muungano Zaelekezwa Kukarabati Barabara
Apr 20, 2026
Fedha Sherehe za Muungano Zaelekezwa Kukarabati Barabara
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameagiza fedha zilizokuwa zimepangwa kwa ajili ya maadhimisho ya Sherehe za Muungano mwaka huu zielekezwe katika ukarabati wa miundombinu ya barabara iliyoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.
Na Mwandishi Wetu - MAELEZO

Dkt. Nchemba ametoa kauli hiyo leo, Aprili 20, 2026 jijini Dodoma, alipokuwa akiuarifu umma kuhusu namna maadhimisho ya miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakavyofanyika.

Amesema uamuzi huo unalenga kuhakikisha rasilimali za Serikali zinatumika moja kwa moja kutatua changamoto zinazowakabili wananchi, hususan katika sekta ya miundombinu iliyoathiriwa na mvua.

“Maadhimisho ya miaka 62 ya Muungano yatafanyika katika ngazi ya mikoa yote nchini, ambapo viongozi wakuu wa kitaifa watashiriki katika shughuli za maendeleo ikiwemo kutembelea miradi, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali,” amesema Dkt. Nchemba.

Hatua hiyo inaakisi dhamira ya Serikali ya kuelekeza matumizi ya fedha katika miradi yenye tija kwa wananchi, huku ikiendelea kuenzi umuhimu wa Muungano kwa vitendo vya maendeleo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi