Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Hospitali ya Benjamin Mkapa Yapongezwa kwa Kuunda Baraza la Wafanyakazi

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainabu Chaula akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Baraza hilo mapema hivi karibuni jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dkt. Alphonce Chandika.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dkt. Alphonce Chandika akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Hospitali hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza hilo mapema hivi karibuni jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainabu Chaula.

Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainabu Chaula (hayupo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza hilo mapema hivi karibuni jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainabu Chaula akikata utepe kuashiria rasmi uzinduzi rasmi wa Baraza la Wafanyakazi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa mapema hivi karibuni jijini Dodoma. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dkt. Alphonce Chandika.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainabu Chaula akimkabidhi Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Bw. Maudhi Mayunga Mkataba wa Utendaji Kazi alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Baraza hilo mapema hivi karibuni jijini Dodoma. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dkt. Alphonce Chandika.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainabu Chaula akimkabidhi Mwakilishi wa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Bi. Asha Mkataba wa Utendaji Kazi katika hafla ya uzinduzi wa Baraza hilo mapema hivi karibuni jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dkt. Alphonce Chandika.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainabu Chaula akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Afya na Serikali Kuu (TUGHE) mkoa wa Dodoma Mchenya John mara baada ya kuzindua Baraza la Wafanyakazi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa mapema hivi karibuni jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainabu Chaula akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa mara baada ya kuzindua Baraza hilo mapema hivi karibuni jijini Dodoma. (Picha na: Frank Shija – MAELEZO)

419 thoughts on “Hospitali ya Benjamin Mkapa Yapongezwa kwa Kuunda Baraza la Wafanyakazi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama