Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

HESLB Yaanza Kuwadai Waliokopeshwa ‘Law School’

Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam

Wanasheria 5,065 waliokopeshwa zaidi ya Shilingi 10.6 kama mikopo wakiwa wanafunzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria Tanzania (Law School of Tanzania – LST) sasa watapaswa kurejesha mikopo hiyo kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).

Wanasheria hawa ni wale walionufaika na mikopo ya elimu wakiwa wanafunzi wa LST kati ya mwaka 2008 na 2015 wakisoma Stashahada ya Juu ya Uanasheria kwa Vitendo (Post Graduate Diploma in Legal Practice) wakati Sheria ya HESLB ilipokua hairuhusu wanafunzi wa LST kukopeshwa. Sheria ya HESLB ilirekebishwa mwaka 2014 na kuruhusu wanafunzi wa LST kukopeshwa na HESLB.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama