Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Hakuna Mwananchi Anayeondoka Loliondo- Mulamula

Na Paschal Dotto-MAELEZO

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema kuwa hakuna mwananchi anayeondolewa Loliondo bali Serikali inawaongezea Wananchi ardhi kwa matumizi yao.

Akizungumza katika Mkutano wa Wizara hiyo na Mabalozi Wanaowakilisha nchi zao, Balozi Mulamula alisema kuwa Serikali imeongeza eneo la matumizi ya ardhi kwa wananchi wa Loliondo kwa kuweka mipaka lakini wananchi wa eneo hilo hawaondoki.

“Hakuna mwananchi anayeondoka Loliondo, kinachoendelea Loliondo ni kuwa Serikali imeweka mipaka kwa kuwaongezea eneo kwa ajili ya matumizi yao ya kiuchumi”, amesema Balozi Mulamula.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama