Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Hakuna Eneo Litaachwa Kwenye Zoezi la Uwekaji wa Anwani za Makazi Nchini – Nape

Na Grace Semfuko,MAELEZO

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye, amesema hakuna maeneo yatakayoachwa kwenye zoezi la uwekaji wa anwani za makazi nchini, na kwamba maeneo yote yenye migogoro sugu ya ardhi na mipaka, na ambayo mpaka sasa hayajapitiwa na zoezi hilo yatasubiri utatuzi wake.

Amesema si kwamba maeneo yenye migogoro yameachwa moja kwa moja katika zoezi hilo, bali yatapewa namba lakini hayatawekewa anwani za makazi, lengo likiwa ni kuharakisha utatuzi wa migogoro hiyo ambayo mingi ni ya muda mrefu.

Ameyasema hayo wakati wa ziara ya kukagua na kuhamasisha mwenendo wa zoezi la uwekaji wa amwani za makazi katika Jiji la Dar es Salaam.

“Kwenye hili zoezi kuna baadhi ya maeneo kwa kweli yana migogoro ya hapa na pale, kuna mahali watu wamekaa maeneo ambayo sio rasmi mfano kwenye vyanzo vya maji, migogoro ya mipaka, katika majeshi na wananchi, wengine wamejenga kwenye maeneo ya jeshi la wananchi, sasa kuna maeneo ambayo kwa makusudi tumeamua kuacha kupeleka anwani za makazi mpaka tukamilishe kusuluhisha migogoro iliyopo,  na ni vizuri wananchi wetu wakatuelewa maana wengine wanahoji mbona hapa pameachwa?, niwahakikishieni kuwa hakuna atakaeachwa”, amesema Nape.

13 thoughts on “Hakuna Eneo Litaachwa Kwenye Zoezi la Uwekaji wa Anwani za Makazi Nchini – Nape

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama