Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Gridi ya Taifa Kuunganishwa Katika Kisiwa cha Maisome

Hafsa Omar- Mwanza

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupeleka umeme wa Gridi ya Taifa katika kisiwa cha Maisome kilichopo Wilaya ya Sengerema, mkoani Mwanza.

Agizo hilo limetolewa, Julai 18, 2021 wakati akiwa kwenye ziara ya ukaguzi wa mradi umeme wa jua unaotekelezwa katika kisiwa hicho.

Akizungumza na wananchi, amesema kuwa suluhisho la kudumu la kutatua tatizo la umeme katika kisiwa hicho ni kuunganishwa na gridi ya Taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama