Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Eng. Ngonyani Akagua Ujenzi wa Barabara Mbande-Kongwa Km 11.71

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kushoto), akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw. Deogratius Ndejembi (kulia), wakati alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Mbande – Kongwa KM 11.71 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma jana.

 

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw. Deogratius Ndejembi (kulia), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kushoto), mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Mbande – Kongwa KM 11.71 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma jana.

Sehemu ya barabara ya Mbande – Kongwa yenye urefu wa KM 11.71 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma jana.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amesema hayo mkoani Dodoma jana, mara baada ya kukagua sehemu ya mradi wa barabara ya Mbande-Kongwa-Mpwapwa yenye urefu wa KM 49.14 ambao ujenzi wake unaendelea na kumuagiza Kaimu Meneja Wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Dodoma Eng. Salome Kabunda kusimamia mradi huo kikamilifu.

“Tutahakikisha fedha za mradi huu zinapatikana kwa wakati ili mradi ukamilike  mapema ikiwa ni mkakati wa kuifungua wilaya hii na kuhuisha fursa za kimaendeleo kwa wananchi wa Wilaya ya Kongwa na Mpwapwa”, amesema Eng. Ngonyani.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kulia), akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Dodoma Eng. Salome Kabunda (kushoto), wakati alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Mbande – Kongwa KM 11.71 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma jana.

Ameongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutafungua fursa za uwezekezaji katika maeneo hayo ikiwemo kurahisisha huduma za usafirishaji wa mazao katika Wilaya hizo.

Naye, Kaimu Meneja wa TANROADS, mkoa wa Dodoma Eng. Kabunda, amemhakikishia Naibu Waziri kuwa watamsimamia Mkandarasi anayejenga barabara hiyo kwa karibu ili ubora wa barabara hiyo uendane na thamani ya fedha.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw. Deogratius Ndejembi (wa pili kushoto), pamoja na viongozi wengine wa Serikali wakikagua barabara ya Hogoro – Kongwa KM 14.57 kwa kiwango cha changarawe wilayani humo, mkoani Dodoma jana.

Aidha, Eng. Kabunda amewataka wananchi wa Wilaya ya Kongwa kushirikiana na mkarandarasi ili kuwezesha ujenzi huo kwenda kwa haraka.

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw. Deogratius Ndejembi ameishukuru Serikali kwa kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwani utachochea maendeleo wilayani humo.

Takribani shilingi Bilioni 7.5 zinatarajiwa kutumika katika sehemu ya kwanza ya mradi huo wa Mbande-Kongwa ambapo KM 5 zitajengwa na zinatarajiwa kumalizika ndani ya miezi nane.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

 

126 thoughts on “Eng. Ngonyani Akagua Ujenzi wa Barabara Mbande-Kongwa Km 11.71

Leave a Reply to sildenafil 20 mg tablet walgreens Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama