Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Eneo la Mradi wa kuzalisha Umeme wa Maji ya Mto Ruhudji Lakaguliwa.

Na Zuena Msuya – Njombe

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja ameiongoza timu ya Wataalamu iliyoundwa kutoka Wizara ya Nishati pamoja Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kukagua eneo la mradi wa kuzalisha Umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Ruhudji.

Timu hiyo iliundwa mahsusi kwa ajili ya kusimamia kazi za awali kabla ya kuanza rasmi kwa utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo ambapo pia itashirikisha Taasisi na Wizara mbalimbali za serikali.

One thought on “Eneo la Mradi wa kuzalisha Umeme wa Maji ya Mto Ruhudji Lakaguliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama