Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Dkt.Ndungulile: JAMAFEST Iwe Kichocheo Ulaji Vyakula vya Asili, Kulinda Afya

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile, akiwekewa mafuta ya kulainisha ngozi yaliyotengenezwa kutokana na matunda alipotembelea Banda la Chuo cha VETA katika Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) linaloendelea Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. (Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)

Na. Paschal Dotto – MAELEZO, Dar es Salaam.

25.09.2019

Naibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndungulie ametembelea Maonesho ya Tamasha kubwa la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) na kusisitiza wananchi kutumia zaidi vyakula vya asili ili kupunguza uwezekano wa kupata magionjwa yasisyo ya kuambukiza.

Dkt. Ndungulie amesisitiza utumiaji wa vyakula vya asili baada ya kutembelea Tamasha hilo jana Septemba 25, 2019 ambapo pamoja na mambo mengine alijionea vitu mbalimbali vikiwemo vyakula vya asili na kuwataka Watanzania kujifunza jinsi ya kutumia kuandaa na kutumia vyakula hivyo ambavyo havina madhara katika mwili.

“Katika Tamasha hili Watanzania wanapaswa kujifunza njia za asili katika kuandaa chakula ambacho kinaweza kuwasaidia kulinda afya zao”, alieleza Naibu Waziri

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile, akiangalia moja ya Batiki kutoka kwa Mjasiriamali ambaye anashiriki Maonesho ya Tamasha la Utamaduni la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMFEST) linaloendelea katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. (Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)

Amesema kuwa masuala ya michezo, sanaa na utamaduni yana uhusiano mkubwa na afya na kuwashauri wasanii kutumia Sanaa kuongelea masuala ya kuimarisha afya kkwa kuwasisitiza wananchi kula chakula bora na kufanya mazoezi ili kufikisha ujumbe kwa Jamii kuhusiana na ulaji bora wa chakula.

Kwa mujibu wa Dkt. Ndungulile, asilimia 30 ya watoto chini ya miaka mitano wana utapiamlo na wamedumaa huku asilimia 10 ya watu wazima wakiwa na lishe iliyopitiliza (vitambi) na asilimia 30 wanapatwa na magonjwa yasiyo ambukizwa ambayo mengi yanatokana na vyakula visivyo bora.

Kwa upande mwingine Naibu Waziri Ndungulile ameipongeza Wizara ya Habari, UtamaDUNI, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuandaa Tamasha hilo kwa mafanikio ambapo washiriki kutoka nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki zimeshiriki. Nchi hizo ni wenyeji Tanzania, Burundi, Kenya, Rwanda na Uganda.

JAMAFEST ni Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki ambalo lilipitishwa katika kikao cha 20 na 23 cha Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kilichofanyika mwezi Machi na Septemba 2012.

Tamasha hili hufanyika mara moja kila baada ya miaka miwili na huzunguka katika nchi wanachama wa EAC. Mpaka sasa Tamasha limekwishafanyika katika nchi za Rwanda (2013) na kuhudhuriwa na washiriki 17,500, Kenya (2015) washiriki 21,000 na Uganda (2017) washiriki 42,600 na sasa linafanyika nchini kuanzia Septemba 21 – 28, 2019.

157 thoughts on “Dkt.Ndungulile: JAMAFEST Iwe Kichocheo Ulaji Vyakula vya Asili, Kulinda Afya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama