Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Dkt. Mwigulu Ateta na Mkurugenzi wa Citi Bank


Scola Malinga na Josephine Majura, DSM


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwingulu Lameck Nchemba, amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka CITI Bank unaosimamia Ukanda wa  Jangwa la Sahara na Mashariki ya Kati , ambapo benki hiyo imeahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika uendelezaji wa miradi ya maendeleo, uwekezaji na kufanya tathimini ya  uwezo wa`nanchi kukopesheka (credit rating).


Dkt. Nchemba amefanya kikao jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa CITI group, Bw. David McD. Livingstone amesema Benki yake inajivunia kufanya kazi na Tanzania katika kufikia agenda yake ya kuwaletea wananchi wake maendeleo ya kiuchumi na kijamii.


Mhe. Dkt. Nchemba. alielezea kuwa wamejadiliana namna ya kuharakisha ukamilishaji wa suala la tathimini ya uwezo wa nchi kukopesheka katika masoko ya kimataifa (credit rating) ndani ya mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo CITI Group ndio  washauri wakuu wa zoezi hilo. 


Alisema kuwa Serikali inaendelea kujadili na kuhakikisha kuwa utekelezaji wa miradi mingine ambayo wao wanahusika moja kwa moja kama vile mradi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na miradi mingine ya maendeleo ambayo Serikali iliwahusisha katika utafutaji wa fedha ili kukamilisha miradi iliyopo kwenye mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama