Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).
Dkt. Kijazi Ataka Maafisa Habari wa Serikali Kutoa Elimu ya Sensa ya Makazi
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Allan Kijazi akiwasilisha mada kuhusu Sensa ya watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23, 2022 na umuhimu wake kwa Maendeleo ya Taifa wakati wa kikao kazi cha 17 cha Maafisa Habari , Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali kinachoendelea leo Jijini Tanga tarehe 12 Mei 2022
Na Munir Shemweta, WANMM TANGA
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Allan Kijazi amewataka Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa Sensa ya Makazi na watu inayotarajia kufanyika Agosti 2022.
Dkt. Kijazi alisema hayo mkoani Tanga tarehe 12 Mei, 2022 wakati akiwasilisha mada kuhusiana na Sensa ya Watu na Makazi kwenye kikao cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kinachoendelea mkoani Tanga.
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi, Mhe. Anna Makinda akizungumza na Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali juu ya maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi na wajibu wa Maafisa hao katika kufanikisha zoezi hilo wakati wa Kikao Kazi cha 17 cha Maafisa hao kinachoendelea Jijini Tanga leo tarehe 12 Mei 2022.