Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Dkt. Kalemani Awacharukia Wanaotoza Bei Kubwa za Umeme


Na. Veronica Simba – Sengerema


Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, ametoa onyo kali kwa wazalishaji binafsi wa umeme wanaowatoza wananchi gharama kubwa tofauti na bei elekezi ya Serikali.


Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kahunda, wilayani Sengerema, Mkoa wa Mwanza, Julai 7, 2020, Waziri alisisitiza kuwa gharama stahiki ya umeme kwa wananchi wote wenye matumizi ya kawaida ni shilingi 100 tu kwa uniti moja.


Alisema, wananchi wanapaswa kutozwa gharama inayofanana katika maeneo yote nchini kwani wote wana haki sawa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *