Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Dkt. Jafo Akutana na Mhe. Mohamed Abulwafa, Wajadili Maandalizi ya Mkutano wa 27 wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP27)

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Misri nchini Tanzania, Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa katika Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam leo Agosti 18, 2022.

Pamoja na mambo mbalimbali, kikao hicho kimezungumzuia maandalizi ya Mkutano wa 27 wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP27) unaotarajiwa kufanyika nchini Misri Novemba mwaka huu.

Dkt. Jafo alisema hii ni heshima kubwa kwa Bara la Afrika kushiriki katika mkutano huo na kwamba ushiriki wa Tanzania utatoa fursa katika kutangaza namna inavyoshirikiana na wadau katika hifadhi ya mazingira.

4,050 thoughts on “Dkt. Jafo Akutana na Mhe. Mohamed Abulwafa, Wajadili Maandalizi ya Mkutano wa 27 wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP27)