Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Dkt. Chaula Aongoza Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Kuandaa Mpango Mkakati wa Utendaji Kazi na Ufuatiliaji

Na Faraja Mpina – WMTH

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt Zainab Chaula ameongoza Menejimenti, Maafisa Waandamizi na Wawakilishi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kuandaa Mpango Mkakati wa utendaji kazi na ufuatiliaji kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, kazi itakayofanyika kwa siku 12 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete, Dodoma.

Dkt. Chaula amesema kuwa maandalizi ya kuandaa mpango huo yalikuwa yamekwishafanyika lakini msukumo mkubwa umetokana na kuundwa kwa Wizara mpya ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari yanayoenda sambamba na mabadiliko ya kimuundo kulingana na mahitaji ya Wizara pamoja na kuongeza uwajibikaji wenye matokeo chanya.

One thought on “Dkt. Chaula Aongoza Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Kuandaa Mpango Mkakati wa Utendaji Kazi na Ufuatiliaji

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama