Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Dkt. Abbasi Aviasa Vyombo vya Habari Kuunga Mkono Mageuzi Yanayoletwa na Serikali

Mkurugenzi wa ABM Fm Bw. Abdalah Majura (Mwenyeshati Jeupe) akimuonesha Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi Chumba cha kurushia matangazo wakati wa ziara yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma.

 

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimsikiliza Mkurugenzi wa ABM Fm Bw. Abdalah Majura (Mwenyeshati Jeupe) wakati wa ziara yake yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma.

Frank   Mvungi-  MAELEZO, Dodoma

Vyombo vya Habari nchini vimeaswa kuunga mkono  juhudi za Serikali  katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo kwa maslahi mapana ya Taifa.

Akizungumza Wakati wa ziara yake yakutembelea Vyombo vya habari leo mjini Dodoma Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan  Abbasi amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maendeleo endelevu kwa kuwa misingi ya Taifa letu imejengwa katika uchumi jumuishi.

“ Kuna umuhimu kwa vyombo vya habari kushiriki kikamilifu kueleza faida za miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa kama ule wa ujenzi wa reli ya Kisasa (Standard Gauge) kwa wananchi ili nao washiriki kikamilifu katika  utekelezaji wake ambapo ukishakamilika utakuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo” Alisisitza Dkt. Abbasi

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na wafanyakazi wa Radio ABM FM wakati wa ziara yake yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma.

 

– Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi Mkurugenzi wa ABM Fm Bw. Abdalah Majura (Mwenyeshati Jeupe) toleo Maalum la Jarida la Nchi Yetu kuhusu mafaniko ya miaka miwili ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akifanya mahojiano maalum na Mkurugenzi wa ABM Fm Bw. Abdalah Majura (Mwenyeshati Jeupe) wakati wa ziara yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma.

Akifafanua amesema kuwa dhamira yakuwaletea wananchi maendeleo inaendelea kutekelezwa kupitia mfumo wa elimu bure, uzalishaji wa umeme wakutosha, Ujenzi wa uchumi wa Viwanda, ujenzi wa miundo mbinu kama barabara, reli na upatikanaji wa huduma muhimu kama madawa ambapo Serikali imeongeza bajeti ili kuhakiksha kuwa kila mwananchi anapata huduma muhimu na za msingi katika ubora unaotakiwa.

Aliongeza kuwa Serikali kwa sasa  imeweka  msukumo na kipaumbele   katika kutoa huduma bora kwa wananchi wote hali inayotoa changamoto kwa vyombo vya habari kushiriki kikamilifu katika kusaidia juhudi hizo ili malengo yake yafikiwe kwa wakati.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Radio ABM FM wakati wa ziara yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma.

 

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwa na Mkurugenzi wa RASI FM Bw. Ramadhani Mkosola (kushoto) wakati wa ziara yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma.

 

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na wafanyakazi wa Radio ya RASI FM wakati wa ziara yake yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma.

 

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akifanya mahojiano maalum na kituo cha Radio cha RASI FM wakati wa ziara yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma.

 

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Radio ya RASI FM wakati wa ziara yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma.

PICHA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO

Katika kutekeleza majukumu yake Dkt. Abbasi amepongeza vyombo vya habari kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika kuleta mageuzi ya kweli.

Aidha Dkt. Abbasi aliviasa vyombo vya Habari kuzingatia weledi katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku ili kuchochea ukuaji wa uchumi na ujenzi wa Tanzania mpya kama ilivyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Ziara ya  Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali katika vyombo vya Habari Mkoani Dodoma ni sehemu ya utaratbu wakutembelea wadau wa sekta ya Habari ili kuimarisha utendaji kazi, ambapo Leo ametembelea vituo vya redio vya ABM fm na RAS fm.

22 thoughts on “Dkt. Abbasi Aviasa Vyombo vya Habari Kuunga Mkono Mageuzi Yanayoletwa na Serikali

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama