Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Dkt. Abbasi Atembelea Mabanda ya Maonesho Wiki ya Viwanda-SADC

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi, akisoma kipeperushi cha badhaa inayozalishwa nan a kampuni ya ushonaji Malika Designer alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya Wiki ya Viwanda kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Viwanja wa Karimjee na Gymkana Jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Mmiliki wa Kampuni hiyo Malika Rashidi.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi, akifafanua Jambo mbele ya wafanyakazi wa Kampuni ya Tanzanitie Founder Foundation, kuhusu kuyatangaza madini ya Tanzanite alipotembelea kwenye Banda hilo katika Maonesho ya Wiki ya Viwanda kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya SADC, yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Viwanja wa Karimjee na Gymkana Jijini Dar es Salaam.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi, akipokea kitabu kinachohusu utafiti na Uchenjuaji Madini kutoka kwa Mhandisi Mchenjuaji Madini Mwandamizi, Priscus Kaspana alipotembelea Banda la Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini –Tanzania katika maonesho ya Wiki ya Viwanda kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya SADC yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Viwanja wa Karimjee na Gymkana Jijini Dar es Salaam.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi, akiwa kwenye picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Wakala wa Vipimo, Ukaguzi wa Bidhaa Zilizofungashwa alipotembelea banda la Taasisi hiyo katika maonesho ya Wiki ya Viwanda kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya SADC yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Viwanja wa Karimjee na Gymkana Jijini Dar es Salaam.

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Ukanda wa Uzalishaji wa Mauzo ya Nje(EPZA), George Karumuna na Zubeda Elias, wakimsikiliza Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi, alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya Wiki ya Viwanda kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya SADC yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Viwanja wa Karimjee na Gymkana Jijini Dar es Salaam.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi, akiangalia moja ya bidhaa ya korosho inayozalishwa hapa nchini na Kampuni ya Tan Korosho alipotembelea Banda la Mkuu Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), katika maonesho ya Wiki ya Viwanda kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya SADC yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Viwanja wa Karimjee na Gymkana Jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bw.Edwin Rutegaruka.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi, akipata maelezo kutoka kwa Ben Mwanantala wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), kuhusu ujenzi na ufanyaji kazi wa reli ya kisasa(SGR) alipotembelea Banda la TRC katika maonesho ya Wiki ya Viwanda kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya SADC yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Viwanja wa Karimjee na Gymkana Jijini Dar es Salaam.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi, akipata maeleo kutoka kwa Meneja Masoko na Uhusiano wa Benki ya Maendeleo (TIB), Saidi Mkabakuli alipotembelea banda la Taasisi hiyo kwenye katika maonesho ya Wiki ya Viwanda kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya SADC yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Viwanja wa Karimjee na Gymkana Jijini Dar es Salaam, katika ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Konnect Wire Sheila Mwapachu.

(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)

212 thoughts on “Dkt. Abbasi Atembelea Mabanda ya Maonesho Wiki ya Viwanda-SADC

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama