Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

DIT Yatoa Mafunzo kwa Walimu Matumizi ya Vifaa vya TEHAMA

 

TAASISI ya Teknolojia ya Dar es Dar es Salaam (DIT) 21- 25 Oktoba 2019 inaendesha mafunzo ya TEHAMA ya siku tano kwa walimu wa shule za serikali nchini.

Lengo la mafunzo hayo ambayo yanajulikana kitaalamu ‘Basic ICT Devices Maintenance and Repair’ ni kuimarisha utunzaji wa vifaa vya TEHAMA ambavyo hutolewa kwa shule mbalinbali nchini na serikali pamoja na wadau wengine, vifaa hivyo ni ambavyo ni pamoja na kompyuta,  printa na vifaa vya mawasiliano.

Mafunzo hayo yanayotolewa na wataalamu wa DIT yamefadhiliwa na Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (UCSAF). Walimu wanaohudhulia mafunzo hayo ni wa shule za Msingi na Sekondari.

“Serikali hutoa vifaa mashuleni kama kompyuta, printa au vifaa vya mawasiliano kupitia UCSAF, imeonekana kuwa ni muhimu vifaa hivyo vikatunzwa vizuri hivyo tutoe mafunzo kwa walimu hawa ili waweze kutunza na kufanya ukarabati,”

“Walimu tuliowapokea hapa ni 540 na mafunzo haya yanaanza leo Jumatatu na yatafungwa Ijumaa, ni mafunzo ya siku tano,” alisema Mratibu wa Mafunzo kutoka DIT, Daudi Mboma.

Walimu hao ni kutoka Dar es Salaam, Morogoro, Iringa, Pwani, Mtwara, Ruvuma, Lindi, Kilimanjaro, Kilimajaro, Arusha, Manyara, Dodoma, Zanzibar na Tanga.

342 thoughts on “DIT Yatoa Mafunzo kwa Walimu Matumizi ya Vifaa vya TEHAMA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama