Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

DAWASA : Operesheni yakudhibiti uvujaji maji yaonesha mafanikio

Na; Mwandishi wetu

Operesheni ya Kudhibiti uvujaji wa maji katika Jiji la Dar es Salaam imenza kuonesha matokeo chanya katika maeneo yote yaliyofikiwa na zoezi hilo linalolenga kuboresha huduma zinazotolewa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA).

Kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka hiyo, zoezi la kudhibiti uvujaji wa maji linaenda sambamba na kubadilisha mabomba chakavu ya mita 18 katika eneo la magomeni na katika maeneo mengine yatakapofikiwa na Operesheni hiyo inayoendelea.

” Leo tumefanikiwa kudhibiti mivujo 155 kwenye bomba dogo la kusambaza maji ambapo 37 ni ya Magomeni na  mingine 103 ni ile iliyokuwa katika mabomba ya kuwaunganishia wateja maji  katika maeneo  DAWASA inakotoa huduma ” inasisitiza taarifa hiyo.

Pia Imefafanua kuwa DAWASA imeendelea na matengenezo ya njia za usambazaji maji lengo likiwa ni kuendelea kuimarisha huduma kwa wananchi na kuendana na Kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kutoa huduma Bora kwa wananchi wote.

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam ( DAWASA) imekuwa ikiendesha zoezi endelevu la kudhibiti uvujaji wa maji ikiwa ni moja ya hatua za kuendelea kuleta mageuzi ya kiutendaji ndani ya Mamlaka hiyo ili dhamira ya kuanzishwa kwake itime kwa wakati.

Operesheni hiyo tayari imefanyika katika maeneo mbalimbali ya Jiji hilo ikiwemo Tegeta na Magomeni ambapo sasa kuna tofauti katika upatikanaji wa maji katika maeneo hayo ambapo umeendelea kuimarika lengo likiwa kuyafikia maeneo yote.

 


FacebooktwittermailFacebooktwittermail