Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Chande: Mkafanye Kazi kwa Kufuata Sheria

Josephine Majura WFM – Dar es Salaam

Serikali imeitaka Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kufanya kazi kwa kufuata sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ya Serikali wakati wa utelekezaji wa majukumu yao kwa maslahi mapana ya Taifa.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano-APC Bunju jijini Dar es Salaam.

“Hii Bodi kazi yake kubwa ni kuweka sera na mikakati itakayoiongoza na kuishauri Menejimenti katika kutekeleza majukumu ya Taasisi kwa kuzingatia sera za Serikali katika kutoa huduma kwa wananchi”, alisema Mhe. Chande.

32 thoughts on “Chande: Mkafanye Kazi kwa Kufuata Sheria

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama