Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Tanzania Yajiweka Mguu Sawa Kuandaa Tuzo za MTV Afrika Mwaka 2023

Na Shamimu Nyaki – WUSM, Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Saidi Yakubu leo Mei 09, 2022 jijini Dodoma ameongoza kikao cha awali kati ya Wizara na Wawakilishi wa Waandaaji wa Tuzo za MTV Afrika kutoka nchini Afrika Kusini kujadili kuhusu Tanzania kuandaa Tuzo za Muziki za MTV (The MTV Africa Music Awards) kwa mwaka 2022/23.

 Katika kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu Yakubu  ameeleza utayari wa wizara kushirikiana na Kampuni hiyo kwa kuwa ni fursa kubwa ya kuitangaza Tanzania hasa katika kipindi hiki ambacho Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan  imeweka juhudi katika kuitangaza nchi ili kuvutia wawekezaji na watalii wengi duniani kuja nchini.

“Kikao cha leo kimetupa fursa ya kuona namna gani Nchi yetu itafaidika na ujio wa Tuzo hizo, tumeona Wasanii wetu watapata nafasi ya kujitangaza na kutangaza Sanaa ya Tanzania  Duniani, Kuna fursa pia ya kutangaza Nchi yetu katika Utalii hivyo tumepokea wazo na tutalijadili na kutoa mrejesho wenye tija”, amesema Naibu Katibu Mkuu Yakubu.

Waziri Nape: Natoa Siku 14 Maafisa Habari Kuhuisha Tovuti za Serikali

Na Immaculate Makilika – MAELEZO

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye amewataka Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali kuhuisha taarifa za Serikali kwenye tovuti za Serikali na mitando ya kijamii ili wananchi waweze kupata taarifa na kujua kinachoendelea kuhusu Serikali yao.

Akizungumza leo jijini Tanga wakati akifungua Kikao cha 17 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali, Waziri Nape amesema kuwa Maafisa Habari wa Serikali ni daraja linalorahisisha mawasiliano kati ya Serikali na wananchi, hivyo ni muhimu kutimiza wajibu wao kwa kuwa na taarifa sahihi za Serikali na kwa wakati katika tovuti za Wizara au Taasisi zao.

Serikali Yaagiza Mikoa, Halmashauri Kuajiri Maafisa Habari

Na Mwandishi Wetu – TANGA

Serikali imeuagiza uongozi wa Mikoa na Halmashauri ambazo hazina Maafisa Habari/Mawasiliano kuhakikisha inawaajiri wataalamu hao ili waweze kuiunganisha Serikali na wananchi.

Kuajiriwa kwa Maafisa Habari/Mawasiliano kwenye mikoa saba na halmashauri 84 kutatimiza maono ya Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambayo inataka wananchi wapate taarifa kuhusu mambo yanayofanywa na Serikali yao.

“Nimesikia changamoto ya kukosekana kwa Maafisa Habari katika baadhi ya taasisi, mikoa na halmashauri, nafasi zipo kwenye mikoa saba, naagiza Wakuu wa Mikoa waajiri Maafisa Habari/Mawasiliano katika mikoa yao,” ameagiza Waziri Nape.

Filamu ya Royal Tour Yazinduliwa Jijini Dar es Salaam

Rais Dkt. Mwinyi Azindua Filamu ya Royal Tour Zanzibar

Rais Dkt. Mwinyi Kuzindua Royal Tour Zanzibar

Na Grace Semfuko MAELEZO- Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa filamu ya royal tour utakaofanyika Jumamosi Mei 7 mwaka huu Visiwani humo.

Filamu hiyo ambayo kwa mara ya kwanza ilizinduliwa New York na Los Angeles- California nchini Marekani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa nchini Tanzania ilizinduliwa Aprili 28 Jijini Arusha ambapo sasa inasubiriwa kwa hamu kubwa kwa wakazi wa Zanzibar.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Zanzibar leo Ijumaa Mei 6, 2022, Mwenyekiti wa Taifa wa Kamati ya filamu ya royal tour, Dkt. Hassan Abbasi amesema uzinduzi wa filamu hiyo Visiwani Zanzibar una tija kubwa kutokana na historia yake katika sekta ya Utalii pamoja na kutoa heshima kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ni mzaliwa wa visiwani humo.

Waziri Mkuu Azindua Mradi wa USAID ‘Afya Yangu’

ev eşyası depolama