Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Imejipanga Kuendeleza Kilimo cha Umwagiliaji-Mhe Mgumba

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali bungeni leo tarehe 17 Aprili 2019 wakati wa Mkutano wa Kumi na Tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma. 

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Katika mpango kabambe wa Tanzania wa kufanya kilimo cha umwagiliaji kuwa kipaombele kikuu yaani ASDP II kauli ya kuwa kilimo ni maji inajipambanua zaidi kwani inazingatia matumizi bora ya ardhi na maji.

Katika kuongeza ufanisi na tija katika kilimo kupitia umwagiliaji Serikali imejipanga vyema kuimarisha sekta ya kilimo kupitia mbinu bora za kilimo cha kisasa ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) ameyasema hayo bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 17 Aprili 2019 wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe Rehema Juma Migila aliyetaka kufahamu Serikali ina mpango gani wa kuendeleza Kilimo cha Umwagiliaji katika Manispaa ya Tabora, kwa kutumia maji kutoka Bwawa la Igombe baada ya ujio wa maji kutoka Ziwa Victoria kufika Tabora.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Waziri Kairuki akutana na Mabalozi wa Nchi Tatu Kuzungumza kuhusu Uwekezaji.

Na.Paschal Dotto-MAELEZO.
Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Angela Kairuki atakutana na wawekezaji kutoka nchi mbalimbali waliowekeza Tanzania ili kujua changamoto zao na kuzifanyia kazi kwa haraka na kuimarisha mahusiano ya nchi hizo na Tanzania katika sekta ya Uwekezaji.

Akizungumza katika mazungumzo mafupi aliyoyafanya leo kwa wakati tafaouti Mabalozi kutoka nchi za Ufaransa, Uholonzi, Norway pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Marekani USAID, Waziri Kairuki alisema kuwa mazungumzo hayo ni chachu ya ushirikiano katika sekta ya uwekezaji nchini.

Katika mazungumzo na Balozi wa Ufaransa nchini, Frederic Clavier, Waziri Kairuki alisema kuwa nchi ya ufaransa na Tanzania zina ushirikiano wa muda mrefu katika sekta mbalimbali ikiwemo ya uwekezaji pamoja na biashara. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Jitihada za Serikali katika Kupunguza Ajali za Barabarani Nchini

Meneja wa Usalama Barabarani toka Shirika la Afya Duniani (WHO), Bibi. Mary Kessy akizungumza wakati wa mafunzo kwa Waandishi wa Habari kuhusu usalama Barabarani leo jijini Dodoma. Mafunzo hayo yanayoratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Kamati ya Kitaifa ya Usalama Barabarani ya Bloomberg Global Initiative chini ya ufadhili wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Na  Immaculate Makilika- MAELEZO

Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali  imeendelea kupunguza ajali za barabarani kwa kutoa elimu kwa umma kuhusu usalama barabarani zinazofanywa na wadau wa usalama barabarani.

Akizungumza  leo jijini Dodoma wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu usalama barabarani, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani na Mwenyekiti wa Kamati ya Bloomberg Deus Sokoni alisema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendeea kutoa elimu kwa umma pamoja na uboreshaji wa miundombinu ili kupunguza ajali na vifo kwa watanzania. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Biashara ya Zao la Kahawa na Mazao Mengine Kuendelea Kupitia Vyama vya Ushirika

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali bungeni leo tarehe 16 Aprili 2019 wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma. 

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo – Dodoma

 

Serikali imeelekeza biashara ya zao la kahawa na mazao mengine kufanyika kupitia Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) badala ya wanunuzi kwenda kwa wakulima moja kwa moja. 
 
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) ameyasema hayo bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 16 Aprili 2019 wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini Mhe Martin Msuha aliyetaka kufahamu kwanini Serikali ilibadilisha mfumo wa ununuzi na uuzaji kahawa kwamba ni lazima kupitia Vyama vya Ushirika vya Msingi pia ni vyama vingapi vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) vimeundwa Wilayani Mbinga kufuatia kubadilishwa kwa mfumo huo.
 
Alisema kuwa utaratibu huo utamuwezesha mkulima kunufaika na kilimo cha kahawa kwa kuzalisha kahawa yenye ubora na kuuzwa kupitia minada ambapo wanunuzi watashindanishwa na hivyo kupelekea mkulima kupata bei nzuri na yenye tija.
 
Mhe Mgumba alisema kuwa Vyama vya Ushirika huanzishwa na wananchi kutokana na mahitaji yao hivyo, kupelekea kuwepo kwa aina mbalimbali za Vyama vya Ushirika kama vile Vyama vya Ushirika wa kilimo na masoko, mifugo, uvuvi, viwanda, nyumba, fedha na madini. Kwa mujibu wa Sheria ya Ushirika Na.6 ya Mwaka 2013.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Serikali Kufanya Mabadiliko Kanuni za Matumizi ya Nyavu Baharini

Na Jacquiline Mrisho

Serikali imepanga kufanya mabadiliko ya kanuni za matumizi ya nyavu upande wa bahari ili wavuvi waweze kutumia nyavu za milimita nane badala ya milimita kumi zilizokuwa zikitumika awali.

Hayo yamesemwa leo, Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi lililohoji kuwa ni lini Serikali itakuwa tayari kufanya utafiti katika eneo la Ziwa Victoria kama inavyofanya upande wa Bahari ili kuweza kuruhusu matumizi ya nyavu za chini ya milimita nane.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Serikali Mbioni Kuanza Mpango wa Uagizaji wa Gesi ya Mitungi kwa Pamoja

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Erasto Simon, akiwasilisha taarifa kuhusu Wakala huo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakati wa Semina ya Wabunge hao iliyohusu Sekta ya Nishati.

Serikali iko katika hatua za awali za kuandaa mpango wa uagizaji wa gesi ya mitungi (LPG) kwa pamoja kama ilivyo kwa mafuta ya Petroli hali itakayosaidia kudhibiti masuala mbalimbali ikiwemo  bei ya gesi hiyo .

Akizungumza wakati wa semina kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyofanyika jijini Dodoma, Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani alisema kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa, wananchi katika maeneo yote nchini wanafikiwa na huduma hiyo, hivyo Serikali itaratibu usambazaji wa gesi hiyo badala ya kuwaachia wauzaji wenyewe kuamua maeneo  wanayotaka kupeleka gesi.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Credit Suisse Bank: Tutaendelea Kuikopesha Tanzania kwa Kuwa Inakopesheka na Mahili Katika Usimamizi wa Miradi

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akiwa na Mkurugenzi wa Masoko ya Kimataifa wa Benki ya Credit Suisse ya Uingereza Bi. Elizabeth Muchemi, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo katika Ubalozi wa Tanzania Mjini Washington ambapo Credit Suisse Bank imeahidi kuongeza mikopo kwa Serikali kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya kimkakati ya Serikali.

Na Benny Mwaipaja, WFM, Washington DC

Benki ya Credit Suisse ya Uingereza imeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuikopesha Tanzania ili kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo baada kuridhishwa na uaminifu wa urejeshaji mikopo kwa wakati pamoja na ubora wa viwango vya miradi inayotekelezwa nchini.

Ahadi hiyo imetolewa Mjini Washington D.C nchini Marekani na Mkurugenzi wa Masoko ya Kimataifa wa Benki hiyo Bi. Elizabeth Muchemi, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, katika mikutano ya kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha na Kimataifa inayoendelea Mjini, Washington D.C.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Rais magufuli Atekeleza Ndoto ya Baba wa Taifa kwa Kuzindua Mji wa Serikali Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mji wa Serikali ulijengwa katika eneo la Mtumba jijini Dodoma leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na baadhi ya viongozi wengine mara baada ya kufunga jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa Mji wa Serikali katika eneo la Mtumba leo jijini Dodoma.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail