Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais Magufuli Atoa Siku 3o kwa Viongozi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Muonekano wa ndani wa handaki ambalo jana Jumatatu (Juni 29, 2020) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wake na mahandaki mengine madogo ambayo yatakamilisha urefu wa kilometa 2.7 katika ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Morogoro hadi Makutupora Mkoani Dodoma.

Na Mwandishi Wetu – MAELEZO

RAIS Dkt. John Magufuli ametoa siku 30 kwa Viongozi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kumsimamia usiku na mchana mkandarasi wa kampuni ya Padiel JV kuhakikisha anakamilisha kwa haraka  kazi ya ujenzi wa barabara ya Kilosa- Dumila yenye urefu wa Kilometa 24.

Akizungumza katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara hiyo leo (Jumatatu Juni 29, 2020), Rais Magufuli alisema hajaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo inayofanywa kasi ya mkandarasi huyo kutokana ujenzi wa barabara hiyo kuchukua muda mrefu kukamilika. Read more

JPM Kiboko Uchumi wa Maendeleo wa Mtwara Corridor Umewezekana

Na Judith Mhina-MAELEZO

Wilaya ya Mtwara ndiyo lango linalofungua maendeleo wa uchumi wa Kusini mwa Tanzania kwa kuunganisha mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma ikiwa ni pamoja na nchi jirani za Malawi, Msumbiji na Zambia  zitakazowezeshwa kwa sehemu kubwa kusafirisha mizigo yao kwa urahisi kupitia bandari ya Mtwara.

Wilaya hiyo, imejipambanua kutokana na uwepo wa gesi ya asili, ugunduzi wa mafuta kwenye ukanda wa bahari, uwepo wa lango kuu la bandari ya Mtwara na barabara za kiuchumi ikiwemo ya Mtwara-Masasi – Songea, itakayosafirisha madini ya chuma na makaa wa mawe kutoka Liganga, Mchuchuma, Ngaka na Kiwira pamoja na mazao ya kimkakati kama korosho na ufuta ambapo shughuli zote hizo zitakuwa  chanzo na chachu ya kuimarisha maendeleo ya uchumi wa Kusini.

Hayo amesema Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Dastun Kyobya  alipofanya mahojiano na Idara ya Habari- Maelezo ofisini kwake  hivi karibuni, ambapo ameonyesha ni kwa jinsi gani Wilaya ya Mtwara yenye Tarafa nane, Kata 56, Vitongoji 744, Vijiji 197, na Mitaa 120 ndani ya halmashauri tatu za Mtwara Mikindani, Nanyamba na Mtwara Vijijini zinazoboresha uchumi wa lango la kanda ya Kusini. Kwa namna moja au nyingine kuboreshwa kwa bandari, miundombinu ya barabara, umeme wa gesi, ujenzi wa hospitali ya rufaa ya kanda kumeimarisha fursa kwa wilaya  hiyo kuwa  lango  kuu  la kuendeleza maendeleo ya uchumi wa Mtwara corridor kupitia miradi ya Export Processing Zone (EPZ) na Special Economic Zone (SEZ).

Read more

Halmashauri Zatakiwa Kutumia Ramani Zinazotolewa na Wizara ya Ardhi

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali Mstaafu, Nicodemus Mwengela wakiangalia ramani ya Mkoa wa Songwe wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofisi ya ardhi ya mkoa huo jana. Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Ardhi, Wilson Ruge.

Na Munir Shemweta, WANMM SONGWE

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula amezitaka halmashauri nchini kutumia ramani zilizoandaliwa na kutolewa na Wizara ya Ardhi kupitia idara yake ya upimaji na ramani kwa kuwa ndiyo yenye jukumu la kutafsiri mipaka ya nchi.

Akizungumza wakati akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali Mstaafu Nicodemus Mwengela ramani mbili za Tanzania pamoja na ile ya Mkoa wa Songwe jana, Dkt. Mabula alisema, Wizara kupitia idara yake ya upimaji na ramani ndiyo yenye mamlaka ya kuandaa na kutoa ramani nchini tofauti na zile zinazotolewa na watu wengine ambazo wakati mwingine zinakuwa na upotoshaji wa mipaka.

Read more

RC Makonda: Kinondoni ni Mfano wa Kuigwa kwa Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo

Na Mwandishi Wetu

Halmashauri za Mkoa wa Dar es salaam zimetakiwa kuiga mfano wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kutumia vyanzo vya mapato ya ndani, Serikali Kuu pamoja na wadau kama ilivyotekelezwa katika Manispaa ya Kinondoni.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili kwa jimbo la Kinondoni na Kawe yenye lengo la kukabidhi miradi  kwa kamati ya siasa ya Mkoa.

Read more

Naibu Waziri Nyongo Apiga Marufuku Vishoka kwenye Soko la Madini Tunduru

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza na wafanyabiashara wa madini (hawapo pichani) kwenye mkutano uliofanyika katika Soko la Madini la Tunduru Mkoani Ruvuma wenye lengo la kusikiliza na kutatua changamoto tarehe 29 Juni, 2020.

Na Greyson Mwase, Tunduru

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amepiga marufuku watu wanaofanya biashara nje ya mfumo wa masoko yaliyoanzishwa maarufu kama vishoka na kuongeza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Naibu Waziri Nyongo ameyasema hayo mapema leo tarehe 29 Juni, 2020 kwenye mkutano wake na wafanyabiashara wa madini katika Soko la Madini Tunduru ikiwa ni sehemu ya ziara yake kwenye soko hilo yenye lengo la kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zilizojitokeza kwenye uendeshaji wa soko hilo.

Read more

Tanzana na Ufaransa Zasaini Mkataba Wenye Thamani ya Bilioni 592

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe. Frederic Clavier wakisaini moja ya Mikataba ya Mkopo nafuu wa shilingi bilioni 592.57 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Nishati ya Umeme unaounganisha Tanzania na Zambia, Mradi wa UmemeVijijini (REA) katika mikoa ya Tanzania Bara na Mradi wa Maji safi na Usafi wa Mazingira katika miji inayozunguka Ziwa Victoria Jijini Mwanza. Anayeshuhudia katikati ni Mwakilishi mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (ADF) Bi. Stephanie Essombe, Jijini Dar es Salaam.

  Na Mwandishi Wetu – MAELEZO

Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) zimetiliana saini mikataba mitatu ya mikopo yenye masharti nafuu yenye jumla ya Tsh. Bilioni 592 kwa ajili ya miradi ya usambazaji wa umeme Vijijini , mradi wa umeme wa kuunganisha Tanzania na Zambia  pamoja  na kukamilisha mradi wa Maji Safi na Maji Taka katika miji inayozunguka Ziwa Victoria .

Read more

Waziri Kalemani Akagua Umeme Nyumba kwa Nyumba

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa kijiji cha Isamilo, Wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza, akiwa katika ziara ya ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme vijijini, Juni 26, 2020

Hafsa Omar – Mwanza

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, amefanya ziara nyumba kwa nyumba katika vijiji vya Usagara na Isamilo wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza, Juni 26 mwaka huu, akikagua kazi ya usambazaji umeme.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Isamilo, Waziri aliwaeleza kuwa lengo lake ni kufahamu idadi ya nyumba ambazo hazijaunganishiwa umeme na kujua sababu zilizofanya nyumba hizo zisiunganishwe ili kutafutia ufumbuzi suala hilo.

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa kwanza-kulia) akizungumza na mmoja wa wakazi wa kijiji cha Isamilo, wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza, Restuta Wilbard, alipokwenda kukagua nyumba yake ili iunganishiwe umeme, akiwa katika ziara ya kazi, Juni 26,2020

“Ndugu zangu wananchi, nimekuwa nikipita kwenye barabara hii mara kwa mara lakini kila nikitupa jicho mkono wa kushoto naona nyumba zenu zote hazina umeme jambo ambalo hatuwezi kulikubali,” alisema.

Akieleza zaidi, alisema kuwa mwanzoni mwa mwaka huu (2020), alitoa agizo nyumba hizo zianze kupelekewa umeme lakini mpaka sasa bado hazina umeme.

Alilitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuwapelekea umeme wananchi hao ndani ya siku saba. Read more

Wakaguzi wa Kemikali Watakiwa Kuboresha Utendaji

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kulia), akiongea na Wakaguzi wa Kemikali (hawapo pichani) wakati akifunga mkutano wa mwaka wa Wakaguzi hao ulioandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na kukamilika tarehe 28 Juni, 2020 katika ukumbi wa NSSF, Ilala, Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko amewataka wakaguzi wa kemikali kwenda kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maagizo ya Bodi ya Wakurugenzi kuhusiana na changamoto za ujazaji wa fomu za maombi ya usajili wa wadau wa kemikali.

Read more

Rais Magufuli Azindua Mradi wa Maji Kibamba-Kisarawe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa ili kuzindua mradi mkubwa wa maji wa Kibamba-Kisarawe katika sherehe zilizofanyika Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani leo tarehe 28 Juni 2020.

 Na Erick Msuya

 Rais Dkt. John Magufuli amezindua mradi mkubwa wa maji wa Kibamba-Kisarawe katika Wilaya ya Kisarawe Mkoani wenye thamani ya Tsh. Bilioni 10.6 ambao umekusudia kuondoa tatizo la ukosefu wa maji lililodumu katika Wilaya hiyo kwa zaidi ya miaka 113 sasa.

Wilaya ya kisarawe sasa inapata maji lita Milioni 6 ukiwa ni mradi wenye dhamani ya bilioni 10.6 fedha za ndani za Dawasco. Read more

ev eşyası depolama