Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

CAG Yakoa Shilingi Bilioni 1.45

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipima joto la mwili kabla ya kuingia katika ukumbi wa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma kwa ajili ya kupokea Taarifa ya CAG kwa Mwaka 2018/2019 pamoja na Taarifa ya TAKUKURU leo tarehe 26/03/2020.

Na Jonas Kamaleki, Dodoma

Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) imeokoa jumla ya Shilingi bilioni 1.45 ambayo ingelipwa kama ada ya ukaguzi kwa makampuni binafsi ya ukaguzi.

Hayo yamebainishwa leo Ikulu ya Chamwino, Dodoma na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Charles Kichere wakati akiwasilisha Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2018/19 kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipima joto la mwili kabla ya kuingia katika ukumbi wa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Kichere amesema ofisi yake imeokoa fedha hizo kwa kutumia wakaguzi wa ofisi yake kukagua mashirika ya umma ambayo baadhi yake ni TANAPA, BOT, SUA, TTCL na TIC.

“ Mheshimiwa Rais ofsi yangu imejipanga kukagua mashirika mengine makubwa kama vile Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro, EWURA, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Tanesco, Chuo Kikuu cha Ardhi, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),” amesema Kichere.

Spika wa Bunge Job Ndugai akipima joto la mwili kabla ya kuingia katika ukumbi wa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Kutokana na uhaba wa watumishi katika ofisi ya CAG, Rais Magufuli ameiagiza Utumishi kutoa kibali cha ajira ya watumishi 25 katika ofisi hiyo.

“CAG nakupongeza sana kwa kuanza kukagua mashirika yetu ya umma kwa kutumia watu wetu, ni kitendo cha kizalendo, umefanya vizuri,” amesema Rais Magufuli

Aidha, Rais Magufuli amemthibitisha aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kumpambana na Rushwa (TAKUKURU), Brigedia Jenerali, John Mbungo kuwa Mkurugenzi MKuu wa TAKUKURU kutokana na kazi aliyoifanya ya kurudisha bilioni 8.8 za wananchi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kutoka kwenye ukumbi wa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma ambapo alipokea Ripoti mbili za Mwaka 2018/2019 kutoka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa PCCB pamoja na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG.

Rais Magufuli amemuhakikishia Mhe. Spika, Job Ndugai kuwa Ripoti ya CAG itawasilishwa bungeni jinsi ilivyo bila kubadilishwa kwa namna yoyote ili ijadiliwe na wabunge kwa mujibu wa sheria.

CAG na TAKUKURU wamewasilisha Ripoti zao leo kwa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu ya Chamwino Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Spika wa Bunge Job Ndugai wakwanza kushoto waliokaa, akifatiwa na CAG Charles Kichere, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo wapili kutoka kulia waliokaa pamoja na Wafanyakazi wa Ofisi ya TAKUKURU na CAG, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

. Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Charles Kichere akisoma Muhtasari wa Taarifa yake ya Mwaka 2018/2019 katika Ikulu ya Chamwino mkoani

6 thoughts on “CAG Yakoa Shilingi Bilioni 1.45

 • August 10, 2020 at 1:32 pm
  Permalink

  I do not even know how I ended up here, but I thought this post was good.
  I do not know who you are but definitely you are going to
  a famous blogger if you are not already 😉 Cheers!

  Reply
 • August 14, 2020 at 5:08 pm
  Permalink

  hey there and thank you for your info – I’ve certainly picked up anything
  new from right here. I did however expertise some technical points using this
  web site, since I experienced to reload the website lots of
  times previous to I could get it to load properly.
  I had been wondering if your web host is OK? Not that I am
  complaining, but slow loading instances times will often affect your placement in google and can damage your
  quality score if ads and marketing with Adwords.
  Anyway I am adding this RSS to my email and can look
  out for a lot more of your respective fascinating content.
  Ensure that you update this again very soon.

  Reply
 • August 25, 2020 at 7:49 pm
  Permalink

  Magnificent goods from you, man. I have understand your stuff previous to and you are just extremely
  magnificent. I really like what you have acquired
  here, really like what you’re saying and the way in which you say
  it. You make it entertaining and you still take care of to keep it wise.
  I can not wait to read much more from you. This is
  actually a wonderful website.

  Reply
 • August 31, 2020 at 12:54 am
  Permalink

  Hey there! I’ve been reading your weblog for a while now and
  finally got the courage to go ahead and give you a shout out from New Caney Tx!
  Just wanted to say keep up the excellent job!

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama