Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Bondia Hassan Mwakinyo Atinga Bungeni Leo

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia Bunge wakati wa kuahirisha Mkutano wa 12 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akijibu swali wakati wa mkutano wa 12 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kikao cha tisa leo Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akijibu swali wakati wa mkutano wa 12 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kikao cha tisa leo Jijini Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Chemba mkoani Dodoma, Mhe. Juma Nkamia wakati wa mkutano wa 12 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kikao cha tisa leo Jijini Dodoma.

Bondia Hassan Mwakinyo akitambulishwa mbele ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongiozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa Mkutano wa 12 kikao cha tisa cha Bunge leo Jijini Dodoma. Wabunge wote kwa pamoja wamekubaliana kumchangia bondia huyo shilingi 20,000 kila mmoja ikiwa ni pongezi kutokana na kuleta heshima kwa taifa kwa kuibuka mshindi katika pambano la raundi 10 la uzito wa super welter dhidi ya bondia namba nane duniani Sam Eggington.

Bondia Hassan Mwakinyo (kulia) akiwa na Meneja wake Mbarook Abdallah maarufu Muba One wakiwa Bungeni leo Jijini Dodoma. Bondia huyo ameingia bungeni leo kufuatia mwaliko maalum wenye lengo la kumpongeza kutokana na kuleta heshima kwa taifa kwa kuibuka mshindi katika pambano la raundi 10 uzito wa super welter dhidi ya bondia namba nane duniani Sam Eggington.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiagana na baadhi ya Wabunge na Mawaziri mara baada ya kuahirishwa rasmi kwa Mkutano wa 12 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Jijini Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akimpongeza Bondia Hassan Mwakinyo kutokana na kuleta heshima kwa taifa kwa kuibuka mshindi katika pambano la raundi 10 zito wa super welter dhidi ya bondia namba nane duniani Sam Eggington alipokutana naye leo Bungeni Jijini Dodoma.

Bondia Hassan Mwakinyo akionyesha Mkanda alioupata kufuatia kuibuka mshindi katika pambano la raundi 10 uzito wa super welter dhidi ya bondia namba nane duniani Sam Eggington alipotembelea Bungeni leo Jijini Dodoma. (Picha na: Frank Shija – MAELEZO).B


FacebooktwittermailFacebooktwittermail