Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Bodi ya Filamu Tanzania toeni elimu ya Maadili ya Kitaaluma kwa Wasanii

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (wapili kushoto) akitoa maagizo kwa uongozi wa Bodi ya Filamu Tanzania leo Jijini Dar es Salaam ya kutoa elimu kwa wadau wa tasnia ya filamu kuzingatia maadili ya kitaaluma wapoigiza kulingana taaluma mbalimbali ilikuzipa kazi zao mvuto, (watatu kulia) ni Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo.

Na Anitha Jonas – WHUSM, Dar es Salaam

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi amegiza uongozi wa Bodi ya Filamu Tanzania kuhakikisha unatoa mafunzo kwa wadau wa tasnia ya filamu katika kuzingatia maadili ya kitaaluma.

Dkt.Possi ametoa agizo hilo leo Jijini Dar es Salaam alipotembelea Ofisi za Bodi ya Filamu Tanzania kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa shughuli zao pamoja na uandaaji wa  Marekebisho ya Kanuni za Sheria ya Bodi ya Filamu na Michezo yakuigiza.

“Kumekuwa na changamoto kubwa kwa baadhi ya kazi za filamu kukosa uhalisia katika maigizo ya kitaaluma haswa pale wanapoigiza kuhusu taaluma mbalimbali mfano  Madaktari,Wanasheria au Wahandisi na hii inapelekea kupoteza mvuto wa filamu hizo,”alisema Dkt.Possi.

Akiendelea kuzungumza Dkt.Possi alisistiza kuwa bodi inapashwa kuandaa mradi utakaosaidia wadau watasnia hiyo kupata elimu na pia kuipaisha tasnia hiyo katika nyanja mbalimbali  ikiwemo ngazi za kimataifa na kuimarisha uandaaji wa kazi hizo kwa kuwa na viwango vyenye ubora.

Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo (wa kwanza kulia) akimweleza Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (wa kwanza kushoto) mpango wa bodi kuwa na pragramu ya kuanzisha filamu bora ya mwezi itakayooneshwa kwa siku moja katika kumbi za sinema kote nchini leo alipomtembelea ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kupata taarifa za uendeshaji wa shughuli taasisi hiyo.

Nae Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Dkt.Kiagho Kilonzo alisema kuwa Bodi inampango wa kuanzisha programu  ya kuwa na filamu ya mwezi ya kitanzania ambapo filamu hiyo itapigiwa kura na watanzania na baada ya kushinda itazinduliwa katika Majumba ya Sinema nchini na kwenye vingamuzi kadhaa nchi nzima na kuonyeshwa siku moja katika muda mmoja lengo ikiwa ni kuzitafutia masoko filamu za kitanzania na kukuza kipato cha wanatasnia wa filamu.

“Bodi inampango wa Kuanzisha Kanzi Data ya Waandaji wa kazi za Filamu,Wasambazaji,Waigizaji,Waongozaji na Waandishi wa Miswada ya Filamu lengo likiwa kupata takwimu zao, ili kuwa na njia rahisi ya kuweza kuwasaidia kiuchumi wadau hawa ili angalau waweze kupata bima ya afya au kuwasaidia kupata mikopo,”alisema Dkt.Kilonzo.

Pamoja na hayo nae Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Joyce Fisoo aliishauri  Bodi kutumia tovuti yake katika kipindi cha kupigia kura filamu bora ya mwezi ili kuweza kuitangaza tovuti hiyo kwa wananchi.

Afisa Maendeleo ya Filamu kutoka Bodi ya Filamu Tanzania Bw.Simon Peter akitoa taarifa ya utekelezaji na majukumu ya Kitengo cha Maendeleo ya kazi za Filamu mbele ya Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (hayupo pichani)  leo jijini Dar es Salaam katika kikao cha ufuatiliaji wa shughuli za bodi.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (wa kwanza kushoto) akizungumza mara baada ya kikao  cha ufuatiliaji wa shughuli za Bodi ya Filamu Tanznia leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Joyce Fisoo (wa kwanza kulia) pamoja na Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo (wa pili kulia).

(Picha zote na WHUSM)

 

 

377 thoughts on “Bodi ya Filamu Tanzania toeni elimu ya Maadili ya Kitaaluma kwa Wasanii

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *