Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Bodaboda, Machinga Wavikubali Vifurushi vya Bima ya Afya

Makamu Mwenyekiti wa Bodaboda Mkoa wa Mwanza Bw. Gerald Nyerembe akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na vifurushi vya bima ya afya Mkoani Mwanza, ambapo alisema wamelipokea vyema suala la vifurushi vya Bima ya Afya kwani ni muhimu kwa afya zao.

Makamu Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Mwanza Bw. Joseph Samwel akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na vifurushi vya bima ya afya Mkoani Mwanza, ambapo alisema suala la vifurushi limekuwa kuwa mkombozi kwa machinga.

Na Mwandishi Wetu

Jumuiya za Wajasiriamali wadogowadogo na Waendesha Bodaboda nchini wamepongeza hatua ya kuanzishwa kwa vifurushi vya bima ya afya ambavyo vimewawezesha katika kupata matibabu ya uhakika pindi wanapoumwa.

Wakiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na vifurushi vya Bima ya Afya viongozi wa jumuiya hizo wamesema ilikuwa ni hitaji lao la muda mrefu la kuhakikisha wanachama wao wanakuwa na uhakika wa matibabu kwa kuwa na bima za afya.

“Tunamshukuru sana Mhe. Rais Magufuli na serikali ya awamu ya tano kwa kuwa na maono ya kuhakikisha machinga nasisi tunakuwa na uhakika wa matibabu, awali ilikuwa ni ngumu sana unaenda hospitali ukiwa na hofu ya gharama lakini kwa sasa tunatembea kifua mbele, tunapata tiba popote nchini kwa vifurushi hivi”-Stephen Lusinde Mwenyekiti wa Machinga Taifa

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya Mhe. Anne Makinda akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na vifurushi vya bima ya afya Mkoani Mwanza, ambapo alisema mpango wa vifurushi umekuja kwa ajili ya kuwajumuisha watanzania wote.

Naye Mwenyekiti wa Bodaboda Taifa Bw. Michael Haule amesema kuwa ujio wa mpango huu wa vifurushi ni uthibitisho kwamba serikali ya awamu ya tano kila mtu ni sawa na ndio maana wao kama bodaboda sasa wamewekewa utaratibu rahisi wa kujiunga na vifurushi vya bima ya afya kwa gharama nafuu kabisa.

“Zamani ilikuwa ni ngumu sana kumkuta bodaboda anamiliki kadi ya bima ya afya, bodaboda wengi wawepoteza maisha kutokana na kukosa huduma bora za matibabu kutoka na ajali, ila kwasasa suala hilo ni historia, bodaboda sasa ni kama wafalme tunajidai na kadi zetu”- Michael.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya Mhe. Anne Makinda akitoa kadi za bima za afya kwa wanachama waliojiunga kwa mpango wa vifurushi, leo Mkoani Mwanza.

Mwenyekiti wa Bodaboda Mkoa wa Mwanza Bw. Gerald Nyerembe alisema kuwa wamelipokea suala la vifurushi kwa kuwa ni muhimu kwa afya zao na wanafarijika sana kwa Serikali kuwatambua kwani bima imekuwa na faida kubwa kwao.

Aidha, Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Mwanza Bw. Joseph Samwel amesema suala la vifurushi limekuja kuwa mkombozi na kuokoa maisha ya wajasiriamali wadogo kwani bila afya hakuna maendeleo hivyo wajasiriamali hawana budi kuliona suala la vifurushi kama mkombozi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya Mhe. Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja wanachama waliojiunga kwa mpango wa vifurushi, leo Mkoani Mwanza.

91 thoughts on “Bodaboda, Machinga Wavikubali Vifurushi vya Bima ya Afya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama