Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Bilioni 2 Kutumika Kuboresha Miundombinu ya Shule 56 za Michezo

Na Shamimu Nyaki – WUSM

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul amesema wizara imetengewa takriban Shilingi Bilioni 2 kwa ajili ya kuboresha miondombinu kwa shule maalumu 56 za michezo.

Mhe. Gekul amesema hayo Agosti 04, 2022 katika Ufunguzi wa Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA uliofanywa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kasssim Majaliwa katika Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi Tabora.

“Sekta ya Michezo inaendelea kukua, na hii ni kutokana na ushirikiano mnaoutoa nyinyi Viongozi wetu wa juu ambao umesaidia kuibua na kukuza vipaji vya wananmichezo”, amesema Mhe. Gekul.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama