Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Bilioni 1.1 Zatengwa Kupambana na Mabadiliko ya Tabianchi

Na Lulu Mussa, Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo ametoa rai kwa watekelezaji na wasimamizi wa Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (Ecosystem Based Adaptation for Rural Resilience – EBARR in Tanzania) unaotekelezwa Kaskazini A – Unguja kuongeza kasi ya uchimbaji wa visima katika eneo la Matembwe ili wakazi wa maeneo hayo waweze kunufaika na maji safi na salama.

Dkt. Jafo ametoa rai hiyo leo 28 Januari 2022 mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika eneo la Matembwe na kuzungumza na watendaji na wasimamizi wa mradi

huo na kuwaagiza kusimamia kazi zote zilizopangwa kutekelezwa na kuhakikisha zinakamilika kwa wakati bila kuomba muda wa nyongeza.

Amesema agenda ya mazingira ni suala linaloigusa dunia kwa sasa na kuainisha kuwa athari za mabadiliko ya tabianchi ni dhahiri na ni mjadala wa kidunia hivyo Ofisi yake itahakikisha inashirikiana na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais (Zanzibar) katika kuibua miradi yenye manufaa kwa pande zote mbili za muungano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama