Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Bashungwa: Tuunge Mkono Bidhaa za Ndani ‘Made In Tanzania

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhuhu bidhaa za kiwanda cha vifaa vya umeme cha Africab Jijini Dar es Salaam kinachozalisha vifaa mbalimbali ikiwemo transfoma, katika mwendelezo wa Ziara ya kutembelea viwanda Jijini Dar es Salaam

Baadhi ya Vifaa vya Umeme vinavyozalishwa na kiwanda cha Africab kilichopo Jijini Dar es salaam, kiwanda hicho kinatengeneza vifaa mbalimbali zikiwemo transfoma na nyaya za umeme.

Na. Eric Msuya

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa amewataka wadau wa Viwanda na Biashara kuendelea kuunga mkono Serikali ya awamu ya tano kwa kuendelea kutoa ajira katika viwanda vidogo na vikubwa ili kupunguza adha ya ukosefu wa ajira kwa vijana Nchini.

Ameyasema hayo leo Jumatano katika mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea Viwanda vilivyopo Jijini Dar es salaam na kutoa rai kwa kwa watanzania kutumia bidhaa zinazotokana na viwanda vya ndani ili kuongeza ajira kwa vijana

Moja ya Transfoma inayotengenezwa na Kiwanda cha Africab kilichopo Jijini Dar es salaam, ambapo Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa alitembelea na kutoa rai kwa watanzania kutumia bidhaa zitokanazo na viwanda vya ndani.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Riziki Shemdoe na wamiliki wa kiwanda kuzalisha vifaa vya Umeme cha Tropical kilichopo Dar es Salaam, Bw.Charles Mlawa na Aloyce Ngowi baada ya kutembelea kiwandani hapo leo Februari 19, 2020 katika Mwendelezo wa ziara ya kutembelea viwanda Jijini Dar es Salaam.

“Hongereni kwa kumuunga mkono Rais wetu Magufuli kwa kuwapa ajira watanzania 150, ambao ni wahitimu wa vyuo mbalimbali  hapa nchini, lakini hata wale walikuwa nyumbani wamekaa bila kazi” alisema Mhe. Bashungwa

Katika Ziara hiyo Mhe. Bashungwa amewapongeza Bwana Charles Mlawa na Aloyce Ngowi ambao ni wamiliki wazawa wa kiwanda cha Tropical kilichopo Jijini Dar es Salaam kinachozalisha Vifaa vya Umeme (Soketi na Transfoma) hapa Nchini kwa lengo la kuunga mkono Serikali kufikia Uchumi wa kati wenye viwanda.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Riziki Shemdoe wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Tropical kilichopo Dar es Salaam, Bw. Aloyce Ngowi walipotembelea kiwandani hapo leo Februari 19, 2020 katika Mwendelezo wa ziara ya kutembelea viwanda Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya mashine za kutengeneza vifaa vya umeme zilizopo katika kiwanda cha Tropical kilichopo Jijini Dar es Salaam kama zinavyoonekana kwenye picha kiwanda hicho kinatengeneza vifaa mbalimbali zikiwemo transfoma, nyaya za umeme na soketi za umeme.

“Nyie ni wazalendo, ni mfano tosha kwa wawekezaji wazawa kwa kufahamu umuhimu wa Serikali kufikia uchumi wa kati, transfoma na nyanya za kupitishia umeme zote zenye ubora sasa zinatengenezwa Tanzania tena mwenge, Dar es Salaam, na sio tena kuagiza kutoka nje ya Nchi” alisema Mhe. Bashungwa

aidha Mhe. Bashungwa alitoa rai kwa wananchi na wadau wa sekta ya Viwanda na Biashara kuendelea kuunga mkono kwa  kununua bidhaa za ndani zinazo tengenezwa na wawekezaji wazawa na wazalendo

Mashine ya kusokota nyaza umeme iliyopo katika kiwanda cha Tropical kilichopo Jijini Dar es Salaam kama inavyoonekana kwenye picha, kiwanda hicho kinatengeneza vifaa mbalimbali zikiwemo transfoma, nyaya za umeme na soketi za umeme.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Riziki Shemdoe wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Tropical kilichopo Dar es Salaam, Bw. Aloyce Ngowi jinsi ya kutengeneza transfoma walipotembelea kiwandani hapo leo Februari 19, 2020 katika Mwendelezo wa ziara ya kutembelea viwanda Jijini Dar es Salaam.

“Niwaombe watanzania kuendelea kuipa kipaumbele neno ‘MADE IN TANZANIA’ utajisikiaje umeenda Nchi za watu ukakuta chombo unachotumia kimewekwa nembo ya Tanzania, hakika ni fahari sana” alisema Mhe. Bashungwa

Naye Mkurugunzi Mkuu wa kiwanda cha Tropical, Ndugu Charles Mlawa ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuwaunga mkono na kuwajali katika kuhakikisha sera na  lengo la kufikia uchumi wa kati Nchini ifikapo 2025, kwani mpaka sasa kiwanda hicho kinapata umeme wa uhakika kutoka Tanesco.

Wafanyakazi kutoka kiwanda cha kutengeneza vifaa vya umeme cha Tropical kilichopo Jijini Dar es Salaam, wakitenegeneza Transfoma baada ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa kutembelea kiwanda hicho katika mwendelezo wa ziara ya kutembelea viwanda Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa, akisalimiana na Mfanyakazi wa kiwanda cha Tropical katika kitengo cha kutengeneza soketi katika kiwanda hicho kilichopo Jijini Dar es Salaam.

Transfoma na Vifaa vingine vya umeme kutoka kiwanda cha Tropical ambapo Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa alitembelea katika mwendelezo wa ziara ya kutembelea viwanda Jijini Dar es Salaam kama vinavyoonekana kwenye picha.

“Nampongeza sana Rais Magufuli kwa kuendelea kutuunga mkono sisi wawekezaji wa ndani, kwetu sisi ni fahari na tutaendelea kuiunga mkono Serikali yetu” alisema Bwan. Mlawa

Waziri Bashungwa katika ziara yake, pia alitembelea kiwanda cha AFRICAB kilichopo Kurasini Jijini Dar es Salaam kinacho jihusisha na utenegezaji wa vifaa vya umeme vya majumbani, kinachomilikiwa na Wageni kutoka India.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail