Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Balozi Mulamula Ashiriki Mkutano wa 12 wa Mawaziri Marafiki wa UN wa Usuluhishi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe Balozi Liberata Mulamula  ameshiriki Mkutano wa 12 wa Mawaziri Marafiki wa Umoja wa Mataifa wa Usuluhishi unaofanyika sambamba na Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York. 

Akizungumza katika mkutano huo Balozi Mulamula amesema usuluhishi ni njia muhimu  katika kutatua changamoto za migogoro duniani na kuusihi Umoja wa Mataifa kuliingiza suala la usuluhishi katika mifumo ya utatuzi wa migogoro ya Umoja wa Mataifa.

Amesema usluhishi ukiingizwa katika mifumo ya utatuzi ya migogoro ya Umoja huo, utasaidia shughuli za upatanishi na utatuzi wa migogoro na hivyo kuufanya Umoja huo kufikia lengo la utatuzi wa migogoro na kuifanya dunia kuwa sehemu salama .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama