Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Balozi Mulamula Apokea Hati za Utambulisho UNHCR, UNFPA

Na Mwandishi wetu, Dar
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula, amepokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Bibi. Mahoua Parums pamoja na Mwakilishi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu (UNFPA) Bw. Mark Bryan Schreiner katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Balozi Mulamula amewaeleza Bibi. Parums na Bw. Schreiner kuwa UNHCR na UNFPA zimekuwa na mchango mkubwa kwa kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kushughulikia masuala ya wakimbizi pamoja na kukuza maendeleo.
“Tumekubaliana na UNHCR kuendelea kushirikiana kwa karibu pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani katika mchakato wa kurudisha wakimbizi wa Burundi nchini kwao kusudi hali ya Burundi iendelee kutengamaa kwani kurudi kwa wakimbizi hao kutachangia maendeleo ya Burundi,” amesema Balozi Mulamula.
Balozi Mulamula ameongeza kuwa itakumbukwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye alipofanya ziara ya kitaifa hapa nchini Oktoba 2021 alitoa rai ya wakimbizi wa Burundi warudi nchini kwao ili kuweza kuchangia maendeleo ya Taifa hilo.  

93 thoughts on “Balozi Mulamula Apokea Hati za Utambulisho UNHCR, UNFPA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama