
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Raymond Mushi wakati akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Dar esb Salaam terehe 8.3.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Raymond Mushi wakati akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Dar esb Salaam terehe 8.3.2015.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Richard Ndassa (katikati) akisisitiza jambo katika eneo la mradi wa kuzalisha umeme kwa njia ya upepo lililopo Kisesile wilayani Singida Mjini mara kamati hiyo ilipotembelea mradi huo ili kujionea maendeleo yake pamoja na kuzungumza na watendaji wa eneo hilo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Richard Ndassa akitoa maagizo kwa Wakandarasi, Wataalamu kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), Wizara ya Nishati na Madini na viongozi mbalimbali kwenye majumuisho ya ziara ya kamati hiyo, baada ya kufanya ukaguzi wa miradi ya umeme mkoani Singida pamoja na kuzungumza na wananchi.
Na Greyson Mwase, Singida
Mkuu wa Kitengo cha Miundombinu na Nishati kutoka Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Pascal Malesa amesema kuwa serikali inatarajia kutumia Dola za Marekani Milioni 132 kwa ajili ya kukamilisha mradi wa kuzalisha umeme wa upepo wenye uwezo wa Megawati 50 ifikapo mapema mwaka 2016.
Malesa aliyasema hayo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyofanya ziara ya kutembelea mradi wa kuzalisha umeme kwa njia ya upepo unaojengwa katika eneo la Kisesile nje kidogo ya Singida Mjini. Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ipo mkoani Singida kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme ili kujionea maendeleo yake pamoja na kuzungumza na wananchi. Read more
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni Machi 7, 2015 akitokea Kigali Rwanda, alikoalikwa na Rais Paul Kagame wa Rwanda kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Eneo la kuhifadhi maji yenye sumu ya kuchenjulia dhahabu katika mradi mmoja wapo uliopo kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga, ni eneo la makazi ya watu ambalo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally N. Rufunga ameufunga rasmi mradi huo na kuagiza mmiliki wake kufikishwa mahakamani kwa kuvunja taratibu za kisheria.
Afisa kutoka ofisi ya madini Mkoa wa Shinyanga akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga juu ya mradi mwingine wa kuchenjua dhahabu eneo la Bushushu katika Manispaa ya Shinyanga