Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Askofu Msonganzila: Tuendelee kumwombea Rais Magufuli

Askofu Michael Msonganzila Jimbo Katoliki Musoma akiongoza ibada ya kumshuruku Mungu kwa kulisaidia taifa kutokupata vifo vingi vya kutokana na virusi vya Corona kama ilivyotabiriwa na mataifa ya nje katika Parokia ya Shirati, ambapo alisisitiza watanzania kuendelea kumuombea Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ili azidi kukua na kuongezeka imani na busara katika kuliongoza taifa, jana wilayani Shirati,mkoani Mara.

 

Na Anitha Jonas – WHUSM,Shirati- Mara.

Watanzania tuendelea kumwombea Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ili aendelee kukua na kuongezeka imani na busara.

Askofu  Michael Msonganzila wa Jimbo Katoliki Musoma ametoa wito huo hivi karibuni katika ibada maalum ya kumshukuru Mungu  iliyofanyika katika Parokia ya Shirati kwa ajili ya kumshukuru mungu kwa kulisaidia taifa dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona tofauti na ilivyotabiriwa na mataifa ya nje nah ii ni kufutia maono Mheshimiwa Rais yaliyosaidia taifa kukabiliana na janga la maambukizi ya Virusi vya Corona.

 “Kwanini tung’ang’ane kupata taarifa za idadi za  vifo, taarifa hizi hazisaidii sana bali  zinaongeza hofu tu na pia hata  taarifa za kweli zinapotolewa baadhi ya watu wanabeza kwa Musoma hii mpaka sasa tunakifo kimoja tu cha mgonjwa wa Corona hakuna taarifa zinazofichwa Kanisa Katolikili lina mfumo wa kupata taarifa kuanzia ngazi ya familia na tunafuatilia ,” alisema Askofu Msonganzila.

 

 

Baadhi ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Shirati wakifuatilia ibada ya kumshukuru Mungu kwa kuliepusha taifa na maambukizi na vifo vingi vya virusi vya Corona kama ilivyotabiriwa na mataifa ya nje iliyokuwa ikiongoza na Askofu Michael Msonganzila Jimbo Katoliki Musoma (hayupo pichani) jana.

Pamoja na hayo askofu huyo alieleza kuwa anafahamu katika kumshukuru mungu makundi mbalimbali ya imani tofauti yalifanya maombi yao na katika Wilaya ya Shirati anafahamu kuwa wapo wazee wa kijadi katika eneo hilo nao walifanya tambiko.

Halikadhalika nae askofu huyo aliendeleea  kusisitiza kuwa pamoja na idadi ya maambukizi kupungua lakini ni vyema wananchi wanaendelea kuzingatia ushauri wa wataalamu wa afya wa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, kuvaa barakoa na kuepuka msongamano.

Kwa upande wa Chifu wa Rorya Ngoje Ogati alisema kuwa tangu janga hilo la virusi vya Corona lilipotangazwa wazee wa eneo hilo  kutoka koo mbalimbali walifanya tambiko la kuzuia ugonjwa huo usifike katika eneo lao na mpaka sasa hakuna mtu hata mmoja katika eneo hilo amepata virusi hivyo.

“Katika ibada yetu ya tambiko tuliyofanya hivi karibuni nilakuzuia maambukizi ya virusi vya Corona katika nchi yote kwa ujumla pamoja na kushukuru kwa eneo la Rorya kutokupata maambukizi kabisa “alisema Chifu Ogati.

Nae Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Dkt.Emmanuel Temu alishukuru  uongozi wa Wilaya ya Rorya kwa kuruhusu makundi yote ya kiimani ikiwemo la wazee wa jadi kufanya ibada ya kushukuru na kuliombea taifa.

 

Baadhi ya viongozi wa Serikali ya wilaya ya Shirati na Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na Askofu Michael Msonganzila Jimbo Katoliki Musoma mara baada ya ibada ya kumshuruku Mungu kwa kulisaidia taifa kutokupata vifo vingi vya kutokana na virusi vya Corona kama ilivyotabiriwa na mataifa ya nje, jana katika Parokia ya Shirati, mwenye tisheti ya mistari ni Mkuu wa Wilaya ya Shirati Saimo Chacha,wa pili kushoto kwa waliyosimama mbele ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Dkt. Emmanuel Temu kuto Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.

Halikadhalika nae mmoja wa wakazi wa Wilaya ya Rorya kutoka Kijiji cha Buturi Bi. Hudo Odemba alisema katika eneo lao hawajawahi kupata maambukizi ya virusi vya Corona na anaamini kuwa matambiko yaliyofanywa na wazee wa eneo hilo yamesaidia kuwakinga pamoja na taadhari wanazochukua za kunawa mikono kwa maji tiririka kila mara.

Baadhi ya Wazee wa Jadi Wilaya ya Rorya wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufanya tambiko la kuliombea taifa dhidi ya janga la virusi vya Corona wakiongozwa na Chifu wa eneo hilo Ngoje Ogati (watano kushoto) na mwenye tisheti ya mistari ni mkuu wa Wilaya ya Rorya Saimo Chacha na (watatu kulia ni) Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Dkt. Emmanuel Temu kuto Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo jana.

4 thoughts on “Askofu Msonganzila: Tuendelee kumwombea Rais Magufuli

 • March 23, 2021 at 9:28 am
  Permalink

  Hi there! I know this is kind of off topic but I was wondering which blog platform are you using for this site?
  I’m getting fed up of WordPress because I’ve had issues with hackers
  and I’m looking at alternatives for another platform.

  I would be great if you could point me in the direction of a
  good platform.

  Reply
 • March 23, 2021 at 7:37 pm
  Permalink

  I am curious to find out what blog system you’re working with?
  I’m experiencing some minor security problems with my latest site and
  I’d like to find something more risk-free.

  Do you have any solutions?

  Reply
 • June 20, 2021 at 5:17 pm
  Permalink

  723760 740290I real delighted to uncover this internet site on bing, just what I was looking for : D also bookmarked . 792482

  Reply
 • June 28, 2021 at 10:20 am
  Permalink

  157792 331063When I initially commented I clicked the -Notify me when new comments are added- checkbox and now each time a remark is added I get four emails with the same comment. Is there any manner you possibly can take away me from that service? Thanks! 39429

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama