Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Almasi Yenye Thamani ya Bilioni 3.2 Yaipaisha Sekta ya Madini Tanzania

Na  Frank  Mvungi

Tanzania imetajwa kuweka historia katika tasnia ya madini baada ya Almasi yenye Karati 512.15 kupatikana hivi karibuni katika eneo la Maganzo Mkoani Shinyanga  na kuuzwa kwa jumla ya shilingi Bilioni 3.2.

Akizungumza katika mahojiano maalum kuhusiana na jiwe hilo,Naibu  Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus  Nyongo amesema kuwa  kutokana na kupatikana kwa almasi hiyo Serikali imepata mapato ya takribani shilingi  milioni 235,000/- kama kodi na tozo mbalimbali ikiwemo mrabaha yamelipwa Serikalini baada ya mauzo hayo.

Madini ya Almasi yenye karati 512.15 kama inavyoonekana katika picha , madini hayao yana thamani ya Bilioni 3.2 yamepatikana katika eneo la maganzo mkoani Shinyanga.

Kuuzwa kwa jiwe hilo moja la almasi katika soko la madini mkoani Shinyanga ni muendelezo wa tija inayopatikana kupitia masoko hayo toka kuanzishwa kwake nchini,jumla ya shilingi bilioni 34.3 zimepatikana kwenye biashara ya dhahabu iliyofanyika katika kipindi cha mwezi mmoja tu kati ya Machi 17 mpaka Aprili 17 Mwaka huu katika masoko ya madini kote nchini,kwa mujibu waziri wa Madini,Doto Biteko,aliyetoa taariga hiyo hivi karibuni.

“Natoa wito kwa wachimbaji wote,madalali na mawakala,kuyatumia ipasavyo masoko hayo kwakuwa kila mmoja atapata stahiki yake tofauti na awali kabla ya kufunguliwa kwa masoko hayo ambapo wachimbaji hawakuwa kwenye mikono salama kufutia kutokua na mfumo rasmi wa uuzaji madini yao”. Alisisitiza Mhe.  Nyongo

Akifafanua amesema kuwa kila mchimbaji anapaswa kuzingatia sheria na Kanuni za sekta ya madini ili kuepuka mkono wa sheria na hatua nyingine ikiwa ni pamoja na kutaifishwa kwa madini yao pale watakapobainika kutaka kutorosha madini ama kujihusisha na magendo.

Aliongeza kuwa baada ya kupatikana kwa almasi hiyo wataalamu wa Wizara hiyo walifanya tathmini ili kuona ubora wake na kiwango kilichopatikana ili kuhakikisha kuwa Serikali inapata mapato yake.

“ Serikali ya Awamu ya Tano imeweka makazo katika kuimarisha sekta ya madini nchini ili itoe mchango unaostahili katika uchumi wetu ndio maana tunaona kuwa kupitia masoko ya madini tuliyoanzisha hata mchimbaji huyu aliyepata hii almasi pale Maganzo aliiuza kupitia soko letu la madini baada ya kufuata taratibu zote” alisisitiza Mhe. Nyongo.

Tanzani ni moja ya nchi zenye utajiri mkubwa wa madini ya aina mbalimbali ikiwemo Almasi, Tanzanite, Dhahabu na mengine mengi.

Serikali ya Awamu ya Tano imeweka mkazo katika kuimarisha sekta ya madini hapa nchini ili iweze kutoa mchango stahiki katika uchumi, kuimarisha sekta ya madini kunaenda sambamba na kuimarisha taratibu za uuzaji wa madini yote yanayozalishwa hapa nchini, kuimarisha usimamizi, kuwawezsha wachimbaji wadogo ili waweze kuchimba kwa tija.

 

 

 

33 thoughts on “Almasi Yenye Thamani ya Bilioni 3.2 Yaipaisha Sekta ya Madini Tanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama