Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

ACACIA Yazikwa Rasmi, Kampui Mpya ya Madini Yaundwa

Na Mwandishi Wetu

Baada ya kampuni yenye utata ya ACACIA kufutwa rasmi, Serikali kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick zimeunda kampuni mpya ya Twiga Minerals Corporation ambayo itasimamia migodi ya Bulynhulu, North Mara na Buzwagi.

Akizunguza wakati wa kutangaza kampuni hiyo mpya leo Oktoba 20, 2019 jijini Dar es Salaam, Rais na Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow amesema kuwa katika uboa huo, Serikali ya Tanzania inamiliki asilimia 16 ya hisa Barrick asilimia 84 za kampuni ya Twiga.

“Makubaliano haya yameanzisha zama moya za ushirikiano na Serikali na tutahakikisha kwamba Tanzania na watu wake wanashiriki kikamilifu katika faida inayopatikana katika migodi. Pia inahitimisha mgogoro wa muda mrefu kati ya Serikali na Acacia ambapo ulisababisha kufungwa kwa mgodi wa North Mara”, alieleza Bristow mbele ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Paramagamba Kabudi.

Amesema kuwa tayari watanzania wameajiriwa na kupata mafunzo kwa ajili ya uendeshaji wa kamouni hiyo mya ya Twiga ambayo sasa inamilikiwa kwa pamoja kati ya Serikali na Barrick.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Paramagamba Kabudi amesema kufuatia kufa kwa kamouniya Acacia, kesi zote ambazo zilifunguliwa na madai dhidi ya Serikali ya Tanzania kuhusiana na Acacia nazo zimekufa.

“Tulivyoanza mazungumzo kuna baadhi ya watu walisema Serikali itashindwa na tutashitakiwa lakini leo hii tumeshinda. Ubia huu umedhihirisha kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli alikuwa na hoja pale alipohoji juu ya utendaji Acacia hapa nchini”, alieleza Profesa Kabudi.

Amesema kuwa makubaliano hayo yana nyaraka tisa ambazo kwa sasa zomepelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya hatua za kisheria na makubaliano hayoyatasainiwa katikatiya mwezi Novemba.

Mazungumzo ya awali kabisa kati ya Serikali na Barrick yalianza Julai 31, 2017 na kumalizika mwezi Octoba kwa makubaliano ya kuifunga kampuni ya Acacia pamoja na ofisi zake zilizoko London, Uingereza. Baada ya hapo kumekuwa na baada ya hapo kumekuwa na mazungumzo kadhaa ambayo yamefikia hatua ya kuundwa kwa kampuni ya Twiga ambayo ni ya ubia kati ya Serikali na Barrick.

7 thoughts on “ACACIA Yazikwa Rasmi, Kampui Mpya ya Madini Yaundwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama