Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wakandarasi Kutoongezewa Muda Miradi ya Umwagiliaji na Ujenzi wa Maghala

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya (Kulia) akikagua ubora wa kifaa cha kutenganishia mifereji ya kupitishia maji ili kuepusha upasukaji wakati alipofanya ziara katika skimu ya umwagiliaji wa Kigugu wilayani Mvomero.

Na Bashiri Salum – Morogoro

Serikali imesema kwa sasa haina mpango wa kuwaongezea muda makandarasi wa miradi ya umwagiliji na ujenzi wa maghala unaofanyika katika Mkoa wa Morogoro chini ya mradi wa kuongeza uwezo wa uzalishaji na tija katika zao la mpunga(ERPP).

Akiongea mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu katika miradi kumi na moja (11) iliyopo mkoani hapo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Gerald Kusaya amesema wakandarasi hao walipewa kazi tangu tarehe 15 Aprili, 2015 na mpaka sasa ipo miradi ambayo haijakamilika.

Awali bwana Benjamini Kiaruzi Mhandisi Skimu ya Umwagiliaji ya Kigugu kutoka Gopa Contractors (T) Ltd ameomba serikali kumpa muda wa nyongeza kutokana na changamoto za uwepo wa mvua nyingi na kucheleweshewa fedha za mapipo ya kwanza na ya pili.

Akijibu maombi ya mhandisi huyo Bw. Kusaya amesema ifikapo tarehe 30 April 2020 serikali itahitaji kupokea miradi yake yote ikiwa tayari na kwa miradi ambazo hazijawa tayari serikali itachukua hatua kulingana na mkataba husika.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya akiwa na wananchi na wataalam mbalimbali wakati wakikagua mfereji mara baada ya kufika katika skimu ya umwagiliaji Kigugu wilayani Mvomero

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya (wa pili kulia) wakati akitoa maelekezo kwa Wahandisi wanaosimamia mradi wa umwagiliaji katika Kijiji cha Kigugu wilayani Mvomero hivi karibuni.

“Mimi sitaki kusikia changamoto nataka kuona wakulima wanakabidhiwa miradi, ni vizuri kufahamu kwamba wakulima wanateseka kwa kusubiri miradi hii ikamilike ili waanze kulima, yapo mazao yanakuka shambani wanashindwa kumwagilia kwa sababu yenu kwa kweli hatutavumilia ikifika mwisho wa AprilI” alisema Gerald Kusaya.

Ameongeza kuwa, mradi ulilenga kujenga maghala matano katika maeneo ambako skimu za umwagiliaji zimeboreshwa kwa lengo la kuhifadhi kabla ya kupatikana soko lenye tija Zaidi alisema Bwana Kusaya.

Hata hivyo amewataka wakulima watakaofaidika na miradi hiyo ikiwemo maghala kushiriki katika ulinzi wa miradi yao ili iweze kudumu kwa muda mrefu na kutafuta njia mbadala ya kuendeleza za namna ya kukarabati miundombinu hiyo kwa kutoa asilimia katika mauzo ya mazao yao.

Ili kuhahikisha usimamizi wa miradi hii unatekelezwa kwa ufasaha Katibu Mkuu ameitaka tume ya umwagiliaji kuhakikisha wanampatia taarifa za kila baada ya siku tatu na kuahidi kwamba atazifanyia kazi mara tu azipatapo.

Miradi hiyo inagharimu Dola za Kimarekani Milioni 16.5 ambapo malengo yake ni kupeleka mbegu mpya za mpunga kwa wakulima,Kukarabati na kuboresha miundombinu ya Skimu 5 za umwagiliaji za Mvumi, Kilangali Seed Farm-ASA, Msolwa Ujamaa, Njage na Kigugu irrigation scheme) ili kuongeza uzalishaji kwa kuzingatia matumizi ya maji yenye ufanisi katika kilimo cha umwagialiaji.

 

244 thoughts on “Wakandarasi Kutoongezewa Muda Miradi ya Umwagiliaji na Ujenzi wa Maghala

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama