Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

RC Dkt. Nchimbi Azindua Maadhisho ya Chakula Duniani Kitaifa Mkoani Singida

Mkuu wa Mkoa wa Singida akihutubia wakazi wa mji wa Singinda a washiriki wa maonesho ya maadhimisho ya siku ya chakula duniani wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa maonesho hayo leo mjini Singida.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wiazara ya Kilimo akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa maadhimisho ya siku ya chakula dunia leo katika viwanja vya Bomberdier mjini Dodoma.

 

Mkuu wa Mkoa wa Singida akizungumza na baadhi ya viongozi mara baada yakuwasili katika viwanja vya Bomberdier kwa ajili ya kuzindua rasmi maadhisho ya siku ya chakula duniani leo mjini Singida.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasilano Serikali, Bw. Revocatus Kasimba (kushoto) akimuelezea jambo Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi(katikati) mara baada ya kumpokea katika viwanja vya Bomberdier tayari kwa kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa maadhimisho ya siku ya chakula duniani yaliyoambatana na maonsesho ya bidhaa za chakua na lishe leo mjini Singida.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Maandalizi ya maadhimisho hayo mara baada ya kuzindua rasmi maadhimisho hayo leo mkoani Singida. (Picha na Idara ya Habari – MAELEZO)

Baadhi ya vikundi vya burudani vikitumbuiza katika hafla ya uzinduzi wa maadhisho ya siku ya chakula dunia.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akionja uji uliopikwa kutokana na unga lishe wa maharage alipotembelea banda la Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi rasmi wa maadhimisho ya siku ya chakula dunia leo mjini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akionja uji uliopikwa kutokana na unga lishe wa maharage alipotembelea banda la Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi rasmi wa maadhimisho ya siku ya chakula dunia leo mjini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Singida akisikiliza maelezo kuhusu namna ya kudhibiti Sumu Kuvu alipotembelea banda la mradi wa kudhibiti sumu kuvu nchini TANIPAC alipkuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi rasmi wa maadhimsho ya siku ya chakula dunia ambayo kitaifa yanafanyika mkoani hum oleo mjini Singida.

Baadhi ya wananchi wakifuatilia hotuba za viongozi wakati wa hafa ya uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya chakula duniani leo mjini Singida.

Msanii wa muziki wa Singeli, maarufu kama Msaga Sumu akitumbuiza katika hafla ya uznduzi wa maadhimisho ya siku ya chakula duniani ambayo kitaifa inafanyika mkoani Singida.

146 thoughts on “RC Dkt. Nchimbi Azindua Maadhisho ya Chakula Duniani Kitaifa Mkoani Singida

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama