Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Jamii Yashauriwa Kutunza na Kuhifadhi Dhana za Jadi

Mwenyekiti wa jamii ya Kwanyama Mvumi Dodoma Mzee Yoram Mgua Mkuya akimsimika uchifu Mzee Henry Chaula Mazengo (mjukuu wa Chifu Mazengo) kuwa Chifu wa pili wa kabila la Wagogo ambaye anachukua nafasi iliyokuwa wazi tangu mwaka 1967 alipofariki Chifu Mazengo tukio lililofanyika Septemba 07 2019 katika kijiji cha Mvumi Dodoma.

Na: Shamimu Nyaki – WHUSM

Jamii imeshauriwa kutunza na kulinda dhana za jadi zinazotambulisha utamaduni ili kuendelea kuenzi na kukuza mila na desturi  ambazo  ndio zinazotambulisha Taifa la Tanzania pamoja na kuweka  kumbukumbu vizuri za jamii hizo.

Ushauri huo umetolewa na Afisa Utamaduni  wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi.Hadija Kisubi katika sherehe ya kusimikwa kwa Chifu wa Kabila la Wagogo Chifu Henry Mazengo  iliyofanyika katika kijiji cha Mvumi Dodoma ambapo amesema kuwa jamii inapaswa kuhifadhi kumbukumbu zote za makabila yao kwakua ndio msingi wa utamaduni wa  nchi.

Bibi Judith Javan Msonjela akimkabidhi vifaa vya uchifu Mzee Yoram Mgua Mkuya akimsimika uchifu Mzee Henry Chaula Mazengo (mjukuu wa Chifu Mazengo) baada ua kusimikwa kuwa Chifu wa pili wa kabila la Wagogo ambaye anachukua nafasi iliyokuwa wazi tangu mwaka 1967 alipofariki Chifu Mazengo tukio lililofanyika Septemba 07 2019 katika kijiji cha Mvumi Dodoma.

Mlezi wa Umoja wa Machifu Tanzania Mzee John Samweli Malecela akitoa baraka kwa Mzee Henry Chaula Mazengo (mjukuu wa Chifu Mazengo) baada ua kusimikwa kuwa Chifu wa pili wa kabila la Wagogo ambaye anachukua nafasi iliyokuwa wazi tangu mwaka 1967 alipofariki Chifu Mazengo tukio lililofanyika Septemba 07 2019 katika kijiji cha Mvumi Dodoma.

“Taifa letu lina mila na desturi nzuri ambazo tunapaswa kuzilinda ,hivyo ni jukumu la kila jamii kuwa na makumbusho ambayo yatahifadhi mila na desturi  lakini pia itasaidia kukuza utalii wa kiutamaduni”alisema Bibi.Hadija.

Ameongeza kuwa Serkali inatambua mchango wa Machifu na viongozi wote wa kimila katika kuelimisha jamii tamaduni ambazo ndio kioo cha Taifa letu hivyo jamii inapaswa kuzingatia ushauri na maelekezo yanayotolewa na Machifu hao.

Awali  Mlezi wa Machifu Tanzania  Mzee John  Malecela amemshauri Chifu aliyesimikwa  Mzee Henry Mazengo kufuata taratibu za kabila hilo katika uongozi wake pamoja na kuendelea kuhimiza watu wa jamii yake kulinda amani ya nchi.

Afisa Utamaduni Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi.Hadija Kisubi akizungumza wakati wa hafla ya kusimikwa uchifu Mzee Henry Chaula Mazengo (mjukuu wa Chifu Mazengo) kuwa Chifu wa pili wa kabila la Wagogo ambaye anachukua nafasi iliyokuwa wazi tangu mwaka 1967 alipofariki Chifu Mazengo tukio lililofanyika Septemba 07 2019 katika kijiji cha Mvumi Dodoma.

Naye Chifu Mazengo ameahidi kulinda mila na desturi za kabila la wagogo ambazo zinaelekea kupotea kutokana na kabila hilo kuingiliana na makabila mengine lakini pia ameomba ushirikiano kwa ajimii yake ili kutimiza majukumu hayo vizuri.

Chifu Henry Mazengo amesimikwa  kuwa Chifu wa pili Septemba 07,2019 kushika nafasi iliyokuwa wazi tangu mwaka 1967 baada ya Chifu wa kwanza wa kabila hilo Chifu Chaula Mazengo kufariki dunia.

6 thoughts on “Jamii Yashauriwa Kutunza na Kuhifadhi Dhana za Jadi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama