Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na wanariadha walioshiriki mbio za Capital City Marathon (hawapo pichani) kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluh Hassan zilizofanyika leo Julai 07,2019 Jijini Dodoma.Kulia ni mratibu wa mbio hizo Bw.Nsolo Mlozi na Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira,Vijana na wenye ulemavu Mhe.Antony Mavunde.

Na Shamimu Nyaki –WHUSM

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe ametoa pongezi kwa watanzania kwa kuwa na mwamko mkubwa wa kupenda michezo kuanzia kushiriki,kushangilia pamoja na uhamasishaji ambao umechangia kwa kiasi kikubwa  mafanikio na  maendeleo ya michezo hapa nchini na uwakilishi mzuri nje ya nchi.

Dkt.Mwakyembe ameyasema hayo leo Jijini Dodoma alipokuwa anamuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluh Hassan katika mashindano ya riadha ya Capital City Marathon ambapo amesema kuwa kwa sasa nchi yetu imeanza kurudi katika ramani ya michezo kutokana na watanzania kushriki kwa wingi katika michezo mbalimbali.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe (aliyeshika filimbi nyekundu) akionyesha ishara ya kuanza kwa mbio za Capital City Marathon kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluh Hassan zilizofanyika leo Julai 07,2019 Jijini Dodoma.

Baadhi ya wanariadha walioshiriki mbio za Capital City Marathon wakijiandaa kuanza mbio zilizofanyika leo Julai 07,2019 Jijini Dodoma.

“Nawapongeza sana Watanzania wamekuwa na ari kubwa sana ya kushirikiki michezo hasa riadha ambayo imetutangaza vyema nje ya nchi,ni matuamini yangu mtaendelea kufanya vizuri zaidi lakini pia na michezo mingine vijana endeleeni kuchezakwa bidii zaidi  kwakua michezo sasa ni chanzo kikubwa cha kipato”amesema Dkt.Mwakyembe.

Aidha Dkt.Mwakyembe ameongeza kuwa Taifa limekuwa na uwakilishi mzuri katika mchezo wa Soka kwani limepata nafasi ya kushiriki AFCON 2019,kuongezeka kwa timu zitakazoshiriki Klabu Bingwa Afrika ambayo ni Simba na Yanga pamoja na Klabu Mbili zitakazoshiriki Kombe la Shirikisho ambazo ni Azam FC na KMC.

Katika hatua nyingine Mhe.Waziri Mwakyembe ameiagiza Idara ya Maendeleo ya Michezo kushirikiana na wadau kuwa na utaratibu wa kuandaa orodha ya wadhamini  wanaojitokeza na namna wanavyodhamini mashindano mbalimbali ili kuweka kumbukumbuku vizuri na kutoa ushauri panapowezekana katika kuimarisha Sekta hiyo.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akimkabidhi zawadi Bw.Rashid Ally baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mbio za Baiskeli Km.22 za Capital City Marathon zilizofanyika leo Julai 07,2019 Jijini Dodoma.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akimkabidhi zawadi Bw.Godlisten Mmmary baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mbio za walemavu za Capital City Marathon zilizofanyika leo Julai 07,2019 Jijini Dodoma.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akimkabidhi zawadi Bw.Emmanuel Giniki baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mbio za Km. 21 kwa wanaume za Capital City Marathon zilizofanyika leo Julai 07,2019 Jijini Dodoma.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akimkabidhi zawadi Bi.Fabiola John baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mbio za Km. 10 kwa wanawake za Capital City Marathon zilizofanyika leo Julai 07,2019 Jijini Dodoma.Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira,Vijana na wenye ulemavu Mhe.Antony Mavunde.

Mratibu wa Mbio za Capital City Marathon Bw.Nsolo Mlozi akitoa neon la shukrani kwa washiriki wa mbio hizo zilizofanyika leo Julai 07,2019 Jijini Dodoma.Kulia ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe(Katikati ) akiwa katika picha ya pamoja na Washindi wa mbio za Capital City Marathon kwa upande wa walemavu pamoja na viongozi wa Mkoa,Chama na Serikali baada ya kumalizika kwa mbio hizo zilizofanyika leo Julai 07,2019 Jijini Dodoma.

Kwa upande wake Mratibu wa Mbio hizo Bw.Nsolo Mlozi mbali na kuishukuru Serikali kwa ushirikiano iliyotoa pamoja na washiriki waliojitokeza  ameishauri jamii kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi na kushiriki mashindano mbalimbali ya riadha ili kujenga miili yao kwa kuimarisha afya lakini pia kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza ambayo kwa sasa yamekuwa yakiwatesa wananchi wengi.

Vilevile Bw.Nsolo ameongeza kuwa Capital City Marathon ilianza na kuwa na idadi ndogo ya washiriki  lakini mwaka huu idadi imeongezeka na kufikia washiriki 2,200 ambao kulingana na miundombinu imara ya Jiji la Dodoma wameweza kukimbia bila kupata changamoto yoyote.

Naye mshindi wa km 21 kwa upande wa wanaume  Bw.Emmanuel Giniki amesema kuwa mchezo wa riadha ni mchezo ambao unahitaji kuwa na mazoezi ya mara kwa mara ili kuweza kufanya vizuri ambapo amewashauri vijana wengi kujitokeza katika mashindano mbalimbali ya riadha yanayotokea ili kupata kipato pamoja na kupata ajira.

Mbio za Capital City Marathon zinafanyika kwa mara ya pili Jijini Dodoma ambapo mwaka huu zimehusisha mbio za KM 22 Baiskeli,km.21wanawake na wanaume,km 10 wanawake na wanaume pamoja na km 5.

236 thoughts on “

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama