Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mil.150 Kukarabati Miundombinu Chuo cha Michezo Malya

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akizungumza na Wahitimu wa Stashahada za Michezo mbalimbali,wanafunzi na wazazi (hawapo katika picha) katika mahafali ya 08 yaliyofanyika Juni 15, 2019 katika Chuo cha Maendeleo ya Micheo Malya kilichopo Wilaya ya Kwimba Jijini Mwanza.Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Bw.Richard Maganga na Kulia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Bw.Jeremiah John.

Na Shamimu Nyaki –WHUSM

Serikali imetenga kiasi cha Shilingi Milioni mia moja hamsini (150,000,000/=) kwa ajili ya kukarabati viwanja pamoja na kuchimba kisima cha maji katika Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya  ili kuondoa kero hiyo iliyodumu kwa muda mrefu chuoni hapo.

Hayo yamesemwa jana  na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza katika mahafali ya nane ya Chuo  hicho ambapo amewataka wahitimu hao kutumia taaluma waliyoipata kuendeleza michezo hapa nchini.

“Fedha hizi ni kwa ajili ya kukarabati miundombinu ambayo Serikali imeelekeza nawaomba sana viongozi mtumie pesa hizi kwa uangalifu na kuzingatia makusudi ya yaliyowekwa  ili changamoto zilizopo ziishe na wanafunzi waweze kusoma katika mazingira rafiki” Mhe.Shonza.

Aidha Mhe.Naibu Waziri ameongeza kuwa Wizara inaendelea kushughulikia andiko lililowasilishwa na chuo hicho la kutaka Chuo kuwa Wakala wa Serikali ili kusaidia kuongeza tija na ufanisi wa chuo hicho ambacho ndio chuo pekee kinachotoa taaluma ya michezo hapa nchini.

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya, Viongozi wa Wilaya ya Kwimba pamoja na baadhi ya Wahitimu wa Stashahada za Michezo mbalimbali, katika mahafali ya 08 yaliyofanyika Juni 15, 2019 katika Chuo hicho kilichopo Wilaya ya Kwimba Jijini Mwanza.

Mhe.Shonza pia amewataka  viongozi na wakufunzi wa chuo hicho kuongeza ubunifu na kutafuta njia mbadala kwa ajili ya kupata fedha za kukabiliana na changamoto mbalimbali pamoja na kukitangaza chuo hicho ili kipate wanafunzi wengi zaidi.

Vilevile amewataka Viongozi wa Halmsahuri ambazo wahitimu wametoka kuwatumia vizuri watalaam hao katika shughuli zote za kimichezo katika maeneo wanayotoka,lakini pia kuongeza idadi ya watumishi kujifunza katika chuo hicho.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Bw. Richard Maganga  amesema kuwa chuo kinatoa mafunzo mbalimbali ikiwemo ya muda mfupi kwa ajili ya kujenga uwezo kwa walimu wa Michezo ambapo mpaka sasa zaidi ya walimu  557 wameshapata mafunzo katika mikoa ya Singida,Mwanza,Dodoma,Iringa,Mbeya na Tabora.

. Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya Bw.Richard Maganga akitoa taarifa fupi ya chuo hicho wakati wa mahafali ya 08 ya Stashahada za Michezo mbalimbali 8 yaliyofanyika Juni 15, 2019 katika Chuo hicho kilichopo Wilaya ya Kwimba Jijini Mwanza.Kulia ni Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza.

“Zoezi hili linafanyika ili kuhamasisha michezo pamoja na kutoa elimu ya awali kwa ajili ya waalimu  wanaofundisha Michezo, Na masomo yanayofundishwa Chuoni hapa  yanazingatia mitaala ambayo imepitishwa na NACTE”Bw.Maganga.

Bw.Maganga ameongeza kuwa tangu Chuo kianze kutoa Stashahada tayari kimeshadahili wanachuo 531 na kimeshatoa wahitimu takriban 280 ambao wengi ni watumishi wa Halmashauri mbalimbali nchini.

Naye Mhitimu Daniel Manala amesema kuwa taaluma aliyopata kwa kipindi cha Miaka miwili itamsaidia katika kufundisha michezo kwa wanafunzi ambao ndio wenye ari kubwa ya kujifunza michezo mbalimbali.

Jumla ya wahitimu 115 wamehitimu mafunzo mbalimbali ikiwemo Stashahada ya ufundishaji michezo,Stashahada ya elimu ya viungo vya mwili katika michezo pamoja na Stashahada ya uongozi na Utawala katika Michezo.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Bw.Jeremiah John akitoa salam za Wilaya wakati wa mahafali ya 08 ya Stashahada za Michezo mbalimbali yaliyofanyika Juni 15, 2019 katika cha Maendeleo ya Michezo Malya Chuo kilichopo Wilaya ya Kwimba Jijini Mwanza. Katikati ni Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza na kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Bw.Richard Maganga

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Bw.Jeremiah John akimkabidhi zawadi Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza aliyopewa na uongozi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya wakati wa mahafali ya 08 ya Stashahada za Michezo mbalimbali yaliyofanyika Juni 15, 2019 katika Chuo kilichopo Wilaya ya Kwimba Jijini Mwanza.

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akikabidhi vyeti kwa baadhi ya Wahitimu wa Stashahada za Michezo mbalimbali, katika mahafali ya 08 yaliyofanyika Juni 15, 2019 katika Chuo cha Maendeleo ya Micheo Malya kilichopo Wilaya ya Kwimba Jijini Mwanza.

 Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akikabidhi vyeti kwa baadhi ya Wahitimu wa Stashahada za Michezo mbalimbali, katika mahafali ya 08 yaliyofanyika Juni 15, 2019 katika Chuo cha Maendeleo ya Micheo Malya kilichopo Wilaya ya Kwimba Jijini Mwanza.

11 thoughts on “Mil.150 Kukarabati Miundombinu Chuo cha Michezo Malya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama