Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mawaziri wa Nishati wa Afrika Mashariki Waahirisha Mkutano Wao

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (kushoto), akiongoza kikao cha ndani baina yake na Wataalamu wa Nishati kutoka Tanzania (hawapo pichani) muda mfupi kabla ya kuahirishwa kwa Mkutano wa 14 wa Baraza la Mawaziri la kisekta la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ufanyike Juni 7, 2019 jijini Arusha. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua.

Na Veronica Simba – Arusha

Mawaziri wenye dhamana na sekta ya nishati kutoka nchi sita zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wameahirisha Mkutano wao uliopangwa kufanyika Arusha, Juni 7 mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa EAC anayeshughulikia Sekta ya Uzalishaji, Jean Baptiste Havugimana, ilieleza kuwa Mkutano huo utafanyika siku nyingine katika tarehe itakayobainishwa na Sekretarieti ya Jumuiya hiyo.

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (Meza Kuu), wakiwa katika kikao cha ndani na Wataalamu wa Nishati kutoka Tanzania, muda mfupi kabla ya kuahirishwa kwa Mkutano wa 14 wa Baraza la Mawaziri la kisekta la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ufanyike Juni 7, 2019 jijini Arusha.

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (katikati) akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kushoto) pamoja na Kaimu Kamishna wa Petroli na Gesi, Mwanamani Kidaya, muda mfupi kabla ya kuahirishwa kwa Mkutano wa 14 wa Baraza la Mawaziri la kisekta la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ufanyike Juni 7, 2019 jijini Arusha.

Katika Mkutano huo, Mawaziri walitarajiwa kupokea, kujadili na kuidhinisha kwa ajili ya utekelezaji, Taarifa ya wataalamu kuhusu miradi mbalimbali ya kisekta, iliyopitiwa na kuidhinishwa na Makatibu Wakuu wa Wizara za Nishati za nchi wanachama wa EAC.

Hata hivyo, Mkutano huo mkubwa wa 14 wa Mawaziri wa Sekta ya Nishati wa EAC, ulifanikiwa kufanyika katika ngazi za awali ambazo huhusisha Wataalamu na kufuatiwa na Makatibu Wakuu.

Vikao vya Wataalamu vilifanyika katika moja ya kumbi za Ofisi za EAC jijini Arusha kuanzia Juni 3 hadi 5 na kukabidhi Taarifa yao kwa Makatibu Wakuu Juni 6, ambao nao walitarajiwa kuiwasilisha kwa Mawaziri husika Juni 7 endapo Mkutano ungefanyika.

Matukio mbalimbali wakati Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua wakiwa katika kikao cha ndani na Wataalamu wa Nishati kutoka Tanzania, muda mfupi kabla ya kuahirishwa kwa Mkutano wa 14 wa Baraza la Mawaziri la kisekta la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ufanyike Juni 7, 2019 jijini Arusha.

Katika Kikao cha Makatibu Wakuu, Tanzania iliwakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua. Aidha, kwa ngazi ya Wataalamu, Tanzania iliwakilishwa na Wizara ya Nishati, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira (Zanzibar), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Wengine ni Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa pamoja (PBPA), Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) na Kampuni ya Kuendeleza Jotoardhi Tanzania (TGDC).

Kabla ya kuahirishwa kwa Mkutano, Mawaziri kadhaa walikuwa wameshafika eneo la tukio akiwemo mwenyeji wao, Dkt. Medard Kalemani (Tanzania), ambaye alifanya kikao cha ndani na Katibu Mkuu Mwinyimvua pamoja na wataalamu Watanzania.

7 thoughts on “Mawaziri wa Nishati wa Afrika Mashariki Waahirisha Mkutano Wao

 • October 26, 2020 at 11:55 am
  Permalink

  I quite like cooking digestech reviews As the human population continues to inch closer to 8 billion people, feeding all those hungry mouths will become increasingly difficult. A growing number of experts claim that people will soon have no choice but to consume insects.

  Reply
 • October 26, 2020 at 8:52 pm
  Permalink

  US dollars atorvastatin 40 mg price cvs Asked how it felt to be a Nobel winner, Englert told reporters by phone link to Stockholm: “You may imagine that this is not very unpleasant, of course. I am very, very happy to have the recognition of this extraordinary award.”

  Reply
 • October 26, 2020 at 9:32 pm
  Permalink

  We need someone with experience where to buy erythritol sweetener in singapore Nothing quite prepares you for the first view of Ragusa Ibla as you round a bend on the road from Modica (whose impressive Ponte Guerreri viaduct features in the opening credits of the main series). There are plenty of handsome old towns in Sicily, but Ibla – the ancient part of a city that was spilt in two by the 1693 earthquake – looks as if a team of masons had carved the place out of a whole hill, like the world’s biggest sandcastle. It’s no less ravishing on the inside.

  Reply
 • October 26, 2020 at 11:11 pm
  Permalink

  Could I make an appointment to see ? cialis 20 mg 30 tablet fiyat Day, one of the nation’s most highly decorated servicemen since Gen. Douglas MacArthur and later a tireless advocate for veterans’ rights, died Saturday surrounded by family at his home in Shalimar, Fla., after a long illness.

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama