Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

PS3 yawezesha mafunzo ya Epicor 10.2 kwa Halmashauri zilizoko nje ya mradi

Wahasibu na Wekahazina kutoka Mikoa ya Tabora na Geita Wakifuatilia Mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma (EPICOR) Toleo la 10.2 mkoani Mwanza.

PS3 haijaziacha nyuma Halmashauri zilizoko nje ya mradi na imewezesha Mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma (EPICOR) toleo la 10.2 yanayoendelea mkoani Mwanza ambapo awamu hii inajumuisha Wahasibu na Wekahazina kutoka Halmashauri zilizomo katika mikoa ya Tabora na Geita.

PS3 inatekeleza mradi kwenye Halmashauri zilizomo kwenye mikoa 13 nchini na ili kuhakikisha kuwa lengo la uimarishaji wa mifumo ya sekta za umma unafikiwa imelazimu kushirikiana na TAMISEMI kwa kutoa mafunzo ya mfumo huu wa Usimamizi wa Fedha za Umma yanafanyika kwa Halmashauri zote nchini.

Godfrey Fwamba, Mhasibu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, mshiriki wa Mafunzo haya amesema kuwa tunashukuru mradi wa PS3 kwa kushirikiana na TAMISEMI kwa kuona umuhimu wa kuwepo kwa mafunzo haya kwa Halmashauri zote nchi nzima na si kwa ambazo mradi unatekelezwan tu. Hii itasaidia Halmashauri zote kwenda sambamba na maboresho yaliyoko kwenye mfumo huu wa EPICOR 10.2 bila kuachwa nyuma.

“Faida kubwa sana ambayo mfumo huu unaenda kutusaidia ni kurahisisha utendaji wetu wa kazi sababu yale yote ambayo tumekuwa tunafanya kwenye madaftari yanaenda kufanyika kielektroniki hivyo tutaweza fanya majukumu mengine kamaa vile kuwahudumia wananchi badala ya kuchukua mda mrefu katika kufanya kazi zetu kama ilivyokuwa hapo awali,” ameongeza Godfrey.

Godfrey Fwamba (Kulia) pamoja na washiriki wengine kutoka Mikoa ya Tabora na Geita wakifuatilia mafunzo ya EPICOR 10.2 mkoani Mwanza.

Mwezeshaji wa Mafunzo haya, Imelda Malima Muhasibu kutoka Halmashauri ya Nzega Mji amesema kuwa EPICOR 10.2 itaenda kuleta mabadiliko makubwa katika Halmashauri hususani kwenye suala la Udhibiti na Usimamizi wa Fedha, hii inatokana na kuwa mfumo huu ulioboreshwa hautaruhusu kufanya matumizi ya fedha tofauti na dhumuni au fungu lililokusudiwa.

Ameongeza kuwa, mfumo huu ulioboreshwa utachochea ufanyaji kazi wa haraka katika kufanya malipo mbalimbali kama vile ulipaji wa wateja wa Halmashauri kama Wazabuni lakini pia na malipo ya ndani kama ya watumishi. Hapo awali mchakato wa kufanya malipo ulikuwa ni mrefu ambapo kwa sasa itachukua hatua chache tu na kuweza kufanya malipo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

182 thoughts on “PS3 yawezesha mafunzo ya Epicor 10.2 kwa Halmashauri zilizoko nje ya mradi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *