Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais Magufuli Aagiza Wizara ya Fedha Kutoa Tsh. Bilioni 2 Ujenzi wa Ikulu Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Ofisi za Ikulu Chamwino Dodoma leo Mei 30, 2020.

 

Jonas Kamaleki

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango kutoa Shilingi bilioni 2 kwa ajili ya kukamilishaujenzi wa Ofisi ya Ikulu, Chamwino, Dodoma.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Ikulu, iliyofanyika leo Chamwino, Dodoma.

Akionyesha kuridhishwa na kazi inayofanywa na SUMA JKT Rais Magufuli amesema kuwa vijana 2400 wanoshiriki ujenzi huo atawafikiria ujenzi utakapokamilika. Read more

“Anga Liko Wazi Tanzania, Watalii Karibuni”- Dkt.Kigwangala

Na. Paschal Dotto

Serikali kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), leo imezindua rasmi filamu inayoitambulisha Tanzania ndani na nje ya nchi katika maeneo mbalimbali ya utalii ambayo inaendana na kauli mbiu ya Tanzania Isiyosahaulika “Tanzania Unforgettable” yenye kuitambulisha Tanzania duniani kote.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Mwenye dhamana ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangala amesema kuwa Tanzania imeendelea kutangaza utalii pamoja na kuwepo kwa ugonjwa wa Covid-19, kwani, Rais Dkt.John Pombe Magufuli ameiongoza vyema nchi katika mapambano bila kuathiri sekta za kiuchumi ikiwemo Utalii.

“Namshukuru Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutuongoza vyema katika mapambano ya covid-19 bila kuathiri sekta za kiuchumi ikiwemo hii ya utalii, kwani kwa  sasa tumefungua sekta hii, kama mnavyojua biashara ni ushindani atakeyewahi kufungua na kuweka misingi mizuri ya kuwahudumia wageni na wahudumu sekta ya utalii ndiye atakayepata faida zaidi, tumeamua kufungua utalii wetu na sasa anga letu lipo wazi kwa watalii”, Dkt.Kigwangala.

Amefafanua kuwa Tanzania imejipanga kuwahudumia vyema watalii watakao watawasili nchini na kuhakikisha kuwa wanaondoka salama ili wakifika katika nchi zao wapeleke habari njema kwamba Tanzania ni salama na watalii ambao walisita kuja waje bila woga.

Amebainisha kuwa Serikali imeamua kufungua sekta ya utalii kwa kufuata tahadhari zote zinazotolewa na mamlaka husika ikiwemo Wizara ya Afya ya Tanzania na Shirika la Afya Duniani (WHO), na kuwakaribisha watalii.

Katika uzinduzi huo, Waziri Kigwangala ametoa rai kwa Watanzania kuisambaza  filamu hiyo kwenye mitandao yao ya kijamii ikiwemo Facebook, Twitter, Instgram, telegram na mitandao mingine, ili iweze kuwafikia walengwa kwa lengo la kutangaza Tanzania kiutalii katika soko la utalii la kimataifa.

“Hii ni video rasmi au filamu fupi kwa lengo la kuitambulisha nchi yetu kiutalii katika soko la utalii kimataifa, na hii imeendana sawa kabisa na kauli mbiu ya Tanzania Unforgettable kwa hiyo ninaomba Watanzania wenzangu tuisambaze kwenye mitandao yetu ya kijamii kwa maana imetafsiriwa katika lugha ya Kiswahili, Kingereza, Kifaransa, Kihispania, Kiisrael na Kichina”, Dkt. Kigwangala.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bi.Devotha Mdachi alisema kuwa Tanzania kwa sasa imejikita zaidi kutangaza vivutio vya utalii kupitia mitandao ya kijamii, kwa hiyo kuzinduliwa kwa filamu hiyo fupi kutawasaidia kuteka soko la ndani na nje ya nchi.

“Sisi Kama Bodi ya Utalii tumejikita zaidi kutangaza utalii kwa kutumia mitandao ya kijamii, kwani mpaka sasa tuna vipindi vinavyoruka mubashara kupitia mitandao yetu kwa mfano kipindi cha Serengeti safari show na kile kinachorushwa na Mamlaka ya Bonde la Ngorongoro, hizi ni moja ya njia za  kutangaza utalii ndani na nje ya nchi”, Bi. Mdachi.

Ameongeza kuwa kupitia filamu hiyo fupi watalii watapata fursa ya kuona utamaduni na maeneo mbalimbali ya kuvutia na kuweza kuchagua sehemu sahihi ya kwenda kutembelea, amewataka Watanzania hasa watu maarufu kusambaza filamu hizo za dakika moja, dakika tatu, dakika saba na dakika 10 kwenye kurasa zao ili ziweze kufika mbali zaidi.

Bilioni 175.6 Kuleta Neema ya Maji Mjini Morogoro

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James akibadilishana hati ya makubaliano ya mkopo wa masharti nafuu na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa hapa nchini, Bi. Stephanie Mouen ESSOMBE, mkopo huo utawezesha Manispaa ya Morogoro kunufaika na mradi wa maji wa Bilioni 175.6

Na Mwandishi Wetu- Dodoma

Shilingi bilioni 175.6 kutatua changamoto ya maji  mjini Morogoro ikiwa ni moja ya hatua za Serikali ya Awamu ya Tano kuwapatia wananchi huduma bora za maji safi na salama katika maeneo yote. Read more

SADC Wapendekeza Kuondolewa kwa Vikwazo vya Kibiashara Mipakani

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge (kushoto) akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Bi. Agnes Kayola wakati akifungua mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC kwa ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika kwa njia ya (Video Conference) leo Jijini Dar es Salaam

Eric Msuya

Katibu Mkuu Wizara  ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge amewataka watanzania kuendelea kudumisha umoja na Ushirikiano wa Kibiashara katika ukanda wa Jumuiya ya maendeleo Kusini mwa Afrika SADC.

Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kufungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC kwa ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika kwa njia ya Mtandao (video conference) leo jijini Dar es Salaam, amesema Mkutano huo ni mahususi kwa kujadili na kuondoa vikwazo vyote vya Kibiashara ili kuweza kuendeleza Uchumi ndani ya Jumuiya.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge (aliyevaa koti jeusi) akiongea na wajumbe wa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC kwa ngazi ya Makatibu Wakuu kwa njia ya (Video Conference) leo Jijini Dar es Salaam

Read more