Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

CRDB yaichangia JKCI Milioni 50 Upasuaji wa Moyo

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa benki ya CRDB Tully Mwambapa akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi mfano wa hundi ya shilingi milioni 50 kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Mwaka jana benki hiyo ilitoa shilingi milioni 50 kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto ambapo hadi sasa imechangia milioni 100.

Read more

BMT Kuandaa Muongozo Kuhusu Ukomo wa Wachezaji wa Nje Nchini

Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Yusuph Singo akifafanua kuhusu usajili wa wanamichezo wa kigeni hapa nchini leo Aprili 29,2020 Jijini Dodoma.

Na Shamimu Nyaki, WHUSM-Dodoma

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limepewa jukumu la kuendelea kuandaaa mwongozo utakaotumika kukusanya maoni kutoka kwa wadau kuhusu ukomo wa wanamichezo wa nje hapa nchini.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Yusuph Singo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ikiwa ni hatua ya kuboresha na kuimarisha sekta ya michezo nchini.

Read more

Majaliwa: Tutaendelea Kuboresha Huduma za Afya

*AKABIDHI MAGARI 10 YA KUBEBEA WAGONJWA KWA WABUNGE 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekabidhi magari 10 ya kubebea wagonjwa kwa wabunge ikiwa ni mwendelezo wa jitihada za dhati za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora za afya karibu na makazi yao.

Magari hayo 10 ni kati ya magari 50 ya kubebea wagonjwa yenye thamani ya sh. bilioni sita yaliyonunuliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Global Fund. Kati ya magari hayo, 18 yatapelekwa kwenye Hospitali za Rufaa za Mikoa na 32 ni kwa ajili ya hospitali za Halmashauri pamoja na vituo vya afya.

Read more

Bodi ya Utalii Yataja Mikakati Endelevu 10 Kuinua Utalii Katika Mlipuko wa Corona

Mwenyekiti wa Bodi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akizungumza na Waandishi wa Habari katika Mkutano wa Bodi uliofanyika Jijini Dar es Salaam Aprili, 29, 2020.

Na Mwandishi Wetu

BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imeainisha mikakati 10 ya muda mrefu inayolenga kuinua soko la utalii nchini ambalo kwa sasa limeathirika na mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu (CORONA) unaosababishwa na kirusi cha (COVID-19) na kuenea katika nchi mbalimbali duniani.

Hayo yamesemwa leo Jumatano (Aprili 29, 2020) Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya (TTB) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo wakati wa mkutano na Waandishi wa vyombo vya habari kuelezea athari za mlipuko ugonjwa wa CORONA na tathimini ya sekta ya Utalii nchini.

Alisema kuwa kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Utalii Duniani (UNWTO), inaonesha kuwa mlipuko wa ugonjwa wa CORONA utasababisha kushuka kwa kiwango cha kati ya asilimia 20-30 ya idadi ya watalii kwa mwaka 2020 pamoja na kusababisha ukosefu wa mapato kiasi cha Dola za Marekani 300-450 Bilioni duniani.

Akifafanua zaidi Jaji Mihayo alisema pia utabiri wa awali uliofanywa na Shirika lisilo la kiserikali linaloshauri nchi na taasisi za kimataifa la DEFC unaonesha kuwa mwenendo wa uchumi duniani umebadilika na utaendelea kubadilika ambapo sekta za utalii na usafiri wa anga ziilizokuwa zimeshamiri, kwa sasa zitakuwa za mwisho kwenye uchangiaji wa ukuaji wa uchumi duniani.

Read more

Majaliwa: Jumla ya Wagonjwa 167 wa Corona Wamepona

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa

*Asema wenye maambukizi wamefikia 480 ikiwa ni ongezeko la wagonjwa 196

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema wagonjwa 167 wamepona ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) na ameendelea kuwasisitiza Watanzania wachukue tahadhari ya kutosha na wafuate ushauri wa Wataalamu wa Afya na maelekezo ya Serikali.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kuanzia tarehe 23 hadi 28 Aprili, 2020 wamepatikana watu wengine wapya wenye maambukizi ya Corona 196 (Bara 174 na Zanzibar 22 ambao walitangazwa na Waziri wa Afya wa SMZ) na kufanya jumla ya wenye maambukizi nchini kuwa 480.

Read more

Miezi Ishirini Yasalia kwa Wanahabari Wasio na Sifa

 

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiwasilisha bajeti ya Wizara hiyo Bungeni jijini Dodoma ambapo imetengewa kiasi cha sh. bilioni zaidi ya 40.1 kwa mwaka huu wa fedha 2020/2021.

Na Eleuteri Mangi, WHUSM-Dodoma

Ni miaka minne tangu Sheria ya Huduma za Habari Namba 12 ya Mwaka 2016 imepitishwa nchini na Bunge mnamo Novemba 5, 2016 na kusainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Novemba 16 mwaka huo huo.

Read more