Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Weledi, Kujituma Ndio Nguzo ya Mafanikio – Dkt. Mwakyembe

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa studio mpya ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) inayojengwa katika eneo la ofisi hizo zilizopo Mikocheni. Programu Tumizi (App) ya Safari Channel pamoja na mfumo mpya wa upashanaji habari unaofahamika kama TBC Aridhio. Hafla hiyo ilifanyika tarehe 30 Machi, 2020 Mikocheni jijini Dar es salaam.

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka watangazaji na watumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuongeza weledi na kujituma ili wengine wapate kuiga mambo mazuri kutoka kwao.

Read more

Naibu Waziri Mabula Aridhishwa na Kasi ya Ujenzi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mara

Jengo la hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mara lililopo eneo la Kwangwa Musoma likiwa katika hatua za ukamilishaji

Na Munir Shemweta, WANMM, Musoma

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara iliyoko Kwangwa Musoma unaogharimu takriban Bilioni 15.082.

Dkt Mabula aliridhishwa na kasi ya mradi wa ujenzi wa hospitali hiyo alipokwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wake jana wakati akiwa katika ziara ya siku moja mkoani Mara.

Alisema, ujenzi wa mradi huo ni ukombozi kwa wananchi wa Mara sambamba na Mikoa na nchi jirani kwa kuwa itakuwa ikitoa huduma za kitabibu kwa wananchi wa maeneo hayo.

Read more

Ofisi ya Ardhi Mara Kuwezeshwa Vifaa vya Upimaji

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akikagua ofisi mpya za ardhi mkoa wa Mara wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi mkoani Mara jana. Kulia kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt. Vincent Naano Anney na Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Mara Jerome Kiwia.

Na Munir Shemweta, WANMM Musoma

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt Angeline Mabula amesema wizara yake itaipatia Ofisi ya Ardhi Mkoa wa Mara vifaa vya upimaji ili viweze kutumiwa na halmashauri za mkoa huo  kwa lengo la kuongeza kasi ya upimaji.

Dkt. Mabula alitoa kauli hiyo jana wilayani Musoma Mkoa wa Mara alipokwenda kukagua ofisi mpya ya ardhi ya mkoa Mara ikiwa ni jitihada za wizara ya ardhi kusogeza huduma za ardhi kwa wananchi.

Awali huduma za ardhi zilikuwa zikitolewa na ofisi za Mkamishna Wasaidizi wa Kanda ambapo kanda moja ilikuwa ikihudumia zaidi ya mikoa miwili jambo lililokuwa likiwapa usumbufu wamiliki wa ardhi kwenda Read more

Wizara Nne Zaunda Kamati Mzee Kisangani Kuwa Bilionea

Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) akiongoza wajumbe wa Wizara nne kwa ajili ya kumsaidia Reuben Mtitu maarufu Mzee Kisangani ambae ni mjasiriamali kutoka wilayani Ludewa aliyeanzisha kiwanda cha kutengeneza zana za madini ya chuma.Issa Mtuwa – Dodoma

Kamati hiyo iliyoundwa Machi 30, 2020 yenye  wataalam 9 kutoka Wizara ya Madini,  Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Wizara ya Viwanda na Biashara na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imeundwa ili kumsaidia Mjasiriamali wa miaka 60 kutoka Mkoa wa Njombe wilayani Ludewa, Reuben Mtitu maarufu Mzee Kisangani ili kutimiza ndoto yake ya kuwa bilionea baada ya kubuni kiwanda kinachotengeneza zana zinazotokana na madini ya chuma.

Read more

Katibu Mkuu Uchukuzi Aridhishwa na Ujenzi wa Chelezo, Meli Mpya na Ukarabati wa Meli Mpya Mwanza

Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho, akitoa maelekezo kwa uongozi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa meli mpya, chelezo na Ukarabati wa Meli ya MV Victoria jijini Mwanza, Mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Eric Hamissi.

Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho, akitoa maelekezo kwa Uongozi wa Kampuni ya KTMI ya Korea Kusini inayofanya ukarabati wa meli Meli ya MV Victoria jijini Mwanza, Mwishoni mwa wiki, wakati alipotembelea maendeleo ya ujenzi wake.

Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho, akimsikiliza Muwakilishi wa Kampuni ya KTMI ya Korea Kusini, inayojenga meli mpya katika bandari ya Mwanza South wakati akimweleza hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa meli, wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea maendeleo ya ujenzi wake mwishoni mwa wiki.

Muonekano wa Chelezo inayojengwa katika bandari ya Mwanza South ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 96. Kukamilika kwa chelezo kutarahisisha matengenezo ya meli katika Ziwa Victoria.

Muonekano wa meli ya MV Victoria mara baada ya ukabati mkubwa ambao mpaka sasa umefikia asilimia zaidi ya 96. Meli hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 1,200 na mzigo wa tani 200.

Wakandarasi Kutoongezewa Muda Miradi ya Umwagiliaji na Ujenzi wa Maghala

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya (Kulia) akikagua ubora wa kifaa cha kutenganishia mifereji ya kupitishia maji ili kuepusha upasukaji wakati alipofanya ziara katika skimu ya umwagiliaji wa Kigugu wilayani Mvomero.

Na Bashiri Salum – Morogoro

Serikali imesema kwa sasa haina mpango wa kuwaongezea muda makandarasi wa miradi ya umwagiliji na ujenzi wa maghala unaofanyika katika Mkoa wa Morogoro chini ya mradi wa kuongeza uwezo wa uzalishaji na tija katika zao la mpunga(ERPP).

Akiongea mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu katika miradi kumi na moja (11) iliyopo mkoani hapo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Gerald Kusaya amesema wakandarasi hao walipewa kazi tangu tarehe 15 Aprili, 2015 na mpaka sasa ipo miradi ambayo haijakamilika.

Read more

Jokate Ateta na Taasisi za Watu Binafsi Kisarawe.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari na Uongozi wa shule ya St.Dorcas(hawapo pichani), kuhusu deni la kodi ya Ardhi takribani milioni 98, ambalo shule hiyo inadaiwa tangu mwaka 2009 hadi sasa, kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Kodi Kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Denis Masami.

Na. E.L. Solla- Wizara ya Ardhi

Kulipa kodi ya Pango la ardhi ni fahari na ni sehemu ya maendeleo ya Taifa kwa ujumla. Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo kama msimamizi wa shughuli za Serikali alipotembelea Taasisi zinazodaiwa kodi ya pango la ardhi Wilayani humo kwa lengo la kujua kwa nini hazijalipa kodi stahiki kwa Serikali.

Katika ziara yake Mkuu huyo wa Wilaya ya Kisarawe aliongozana na Mkuu wa Kitengo cha Kodi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ndugu Denis Masami ambaye alisema kodi ya pango la ardhi ni mojawapo ya sifa za umiliki ardhi. Aliongeza kwamba mtu anaweza kupoteza sifa ya umiliki ardhi pale anapovunja masharti ya umiliki ikiwa ni pamoja na kutokulipa kodi ya pango la ardhi kwa mujibu wa sheria.

Read more

Dkt. Kalemani Asema Corona Isiwe Kisingizio cha Kutokamilisha Miradi ya Umeme

Na Zuena Msuya, Geita

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya usambazaji wa umeme vijijini, kujikinga na kuchukua tahadhari dhidi ya virusi vya Corona ili kuendelea kutekeleza miradi hiyo na kuikamilisha kwa wakati unaotakiwa kwa mujibu wa mikataba.

Dkt. Kalemani alisema hayo, Machi 26, 2020, wakati akiwasha umeme katika Kituo cha Afya cha Bwina, kuwasha taa za barabarani zinazotumia mwanga wa jua ( Solar) na kuwahamasisha wananchi kuendelea kuchukua tahadhari na kujikinga dhidi ya virusi vya Corona katika Wilaya ya Chato mkoani Geita.

Read more

ev eşyası depolama