Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Nchi za SADC Kuweka Sheria ya Kusimamia Miradi ya Kimkakati ya Sekta ya Nishati

Kamishina wa Mafuta na Gesi kutoka Wazira ya Nishati, Bw.Adam Zuberi akiendesha Mkutano wa Wataalam wa Sekta ya Nishati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika Leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Mkurugenzi wa Miundombinu Sekritarieti ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Bi. Mapolao Rosemary Makoena akiwa kwenye Mkutano wa Wataalam wa Nishati kutoka nchi wanachama ulimalizika leo Februari 28, 2020 JNICC Jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Na Mwandishi Wetu

KAMATI ya Wataalamu wa Nishati katika Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imependekeza mataifa hayo kuwa na sheria rasmi za kusimamia miradi ya kimkakati katika sekta ya nishati ili kuwa na utoshelevu wa uhakika wa nishati ya umeme kwa ajili mahitaji ya wananchi wake.
Hayo yamesemwa leo Ijumaa (Februari 28,2020) Jijini Dar es Salaama na Kamishna wa Petroli na Gesi katika Wizara ya Nishati,Adam Zuberi wakati akifunga mkutano wa siku nne wa Kamati ya Wataalamu wa Nishati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kilichoanza tarehe 24-28 Februari mwaka huu.Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Tanzania Read more

Serikali Yapongezwa Kwa Hatua za Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia

 

Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda akisisitiza jambo wakati akifungua Kongamano la Uzinduzi wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Wanawake Duniani Jijini Dodoma Februari 27, 2020.

Serikali ya Tanzania imepongezwa kwa hatua inazochukua katika kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia hapa nchini.

Akizungumza wakati akifungua  Kongamano la   Uzinduzi wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Wanawake Duniani   Jijini Dodoma Februari 27, 2020, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda amesema kuwa Serikali imechukua hatua zilizosaidia kupunguza vitendo hivyo.

“ Serikali imechukua hatua za makusudi kutoa elimu bure, mikopo kwa akina mama, vijana na walemavu ili kuleta ustawi wa wananchi na kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia”,Alisisitiza Mhe. Makinda Read more

TBS Yatoa Elimu kwa Wafanyabiashara na Wawekezaji

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

WADAU wa mikutano ya mashauriano kati ya Serikali, wafanyabiashara na wawekezaji wameendelea kupatiwa elimu kuhusiana na majukumu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS), fursa ya wajasiriamali kupatiwa bure alama ya ubora pamoja na kuzipatia ufumbuzi wa changamoto zinawakabili.

Mikutano hiyo ya mashauriano kwa Mikoa ya Kanda ya Ziwa inayojumuisha Mara, Simiyu, Shinyanga na Mwanza ilianza Jumatatu, Februari 24, mwaka huu na kuhudhuriwa na mawaziri na manaibu waziri zaidi ya nane ikiwa ni mwendelezo wa mikutano iliyotangulia inayolenga kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili wafanyabiasha na wawekezaji.

Mkutano wa majumuisho ya mikutano hiyo ya Kanda ya Ziwa ulifanyika jana jijini Mwanza. Katika mikutano hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Yusuf Ngenya, alitoa elimu kwa wadau hao kuhusu fursa wanazopata wafanyabiashara na wazalishaji ambao bidhaa zao zimekidhi viwango vya ubora, kuhamasisha wajasiriamali kuthibitisha ubora wa bidhaa zao bure pamoja na kuzipatia majibu changamoto wanazokumbana nazo wadau mbalimbali.

Read more

Jenerali Mabeyo Azindua Makao Makuu ya JKT Chamwino Dodoma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo akikata utepe kuzindua Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilayani Chamwino mkoani Dodoma leo Februari 26, 2020.

Na Frank Mvungi

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo amezindua Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.

Akizungumza leo Februari 26, 2020 wakati akizundua makao makuu hayo Jenerali Mabeyo amesema kuwa, JKT imekuwa yakupigiwa mfano kwa utendaji unaotokana na utekelezaji mzuri wa miradi yote waliyokabidhiwa. Read more

Tanzania Yaihakikishia Jumuiya ya Kimataifa Uchaguzi Huru na wa Haki

 

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) (katikati aliyeshika kalamu) akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Bi Patricia Scotland. Kushoto kwa Prof. Kabudi ni Balozi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Geneva,Uswisi Balozi Maimuna Tarishi pamoja na Wakurugenzi na Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Jumuiya hiyo zilizopo Geneva,Uswisi

Tanzania imesema hatua zote ambazo zimechukuliwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufanya mabadiliko katika sheria za vyama vya siasa,sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali na ile ya vyombo vya habari ina lengo la kuimarisha uwajibikaji na uwazi pamoja na kuhakiskisha misingi na tunu za Taifa zinaheshimiwa na kuendelezwa.

Akihutubia katika Kikao cha 43 cha Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linaloendelea Geneva nchini Uswisi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ameihakikishia Jumuiya ya Kimataifa kuwa Tanzania  inaheshimu na itaendelea kuheshimu haki zote binadamu zikiwemo za kisiasa na kwamba sheria zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zina lengo jema la kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa Taifa lenye amani,umoja na utulivu. Read more

Naibu Waziri Mabula Ataka Halmashauri Kutenga Maeneo ya Uwekezaji

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza katika kikao cha Mashauriano baina ya Serikali na sekta binafsi kilichofanyika mkoani Simiyu jana.

Na Munir Shemweta, WANMM SIMIYU

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amezitaka halmashauri nchini kuanza kupanga maeneo ya uwekezaji katika sehemu ambazo miji inakuwa kwa kasi.

Dkt Mabula alisema hayo jana katika mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali na sekta binafsi kuhusiana na changamoto za uwekezaji katika mkoa wa Simiyu.

Alisema, kuna maeneo mengi nchini ambayo miji inaendelea kwa kasi hivyo halmashauri kupitia Wakurugenzi wake zinapaswa kuhakikisha zinatenga maeneo ya uwekezaji kwa lengo la kumuwezesha Mwekezaji atakapopatikana asipate tabu.

‘’Ni vizuri katika kipindi hiki ambacho baadhi ya miji inakuwa kwa kasi halmashauri zikatenga maeneo ya uwekezaji na kuyahaulisha kwa lengo la kuwarahisishia wawekezaji watakapokuja kuwekeza katika halmashauri husika’’ alisema Mabula Read more