Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais Magufuli Azindua Nyumba za Maafisa na Maaskari Magereza Ukonga Dar.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akikata utepe kufungua rasmi nyumba za Maafisa na Askari wa Jeshi la
Magereza Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam kwenye sherehe ya
kukabidhi nyumba hizo kwa Jeshi la Magereza leo Alhamisi Januari 23,
2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akikagua baada ya kufungua rasmi nyumba za Maafisa na Askari wa Jeshi
la Magereza Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam kwenye sherehe ya
kukabidhi nyumba hizo kwa Jeshi la Magereza leo Alhamisi Januari 23,
2020

Na Mwandishi Wetu, MAELEZO, DAR ES SALAAM

23.1.2020

RAIS Dkt. John Magufuli amelitaka Jeshi la Magereza Nchini kutathimini utendaji kazi wake kutokana na mwenendo usioridhisha wa jeshi hilo katika kutekeleza miradi mbalimbali inayopewa na Serikali.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Nyumba za Makazi ya Maafisa na Askari wa Jeshi hilo, leo (Alhamisi Januari 23, 2020) Ukonga Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema ameshangazwa na kasi isiyoridhisha ya utekelezaji wa miradi katika jeshi hilo licha ya kuwa na ukubwa wa kambi 129 nchini.

Akitolea mfano Rais Magufuli alisema Jeshi la Magereza lina jumla ya kambi 129 huku Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) likiwa na kambi 24 tu, lakini ameshangazwa na Magereza kujengewa nyumba za askari wake na JKT huku akishindwa kutumia nguvu kazi ya wafungwa walionao katika magereza mbalimbali nchini.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Waziri Mhagama Atoa Miezi Miwili Mabaraza ya Wafanyakazi Yasiyo Hai Kuhuishwa

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akihutubia Wafanyakazi wa Ofisi wa Taifa ya Takwimu alipokuwa akifungua Mkutano wa Tatu wa Baraza la Tano la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo uliofanyika kwenye leo tarehe 23 Januari, 2020 Jijini Dodoma.

Na Jacquiline Mrisho

Mabaraza ya Wafanyakazi yasiyo hai yaliyopo katika Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali yametakiwa kuhuishwa na kuanza kutekeleza majukumu yake yalioainishwa kisheria.

Agizo hilo limetolewa leo jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alipokuwa akifungua Kikao cha Tatu cha Baraza la Tano la Wafanyakazi la Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Bilioni 23.5 Zaokolewa na TANESCO  Kila Mwaka

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Dkt. Tito Mwinuka akizungumza na akizungumza na waandishi wa habari leo, Jijini Dodoma

Na  mwandishi wetu – Dodoma

Shilingi Bilioni 23.5 zinaokolewa kila mwaka baada ya Serikali kupitia Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kuzima mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta mazito.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya Shirika hilo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya tano, Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo Dkt. Tito Mwinuka amesema kuwa Shirika hilo limefanikiwa kujiendesha bila kupokea ruzuku  kufuatia hatua zilizochukuliwa na Serikali ikiwemo kuzimwa kwa mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Maendeleo ya Ujenzi wa Barabara za Juu katika Makutano ya Ubungo yafikia asilimia 65

Maendeleo ya Ujenzi wa Barabara za Juu katika Makutano ya Ubungo (Ubungo Interchange). Mradi huo wa Ujenzi katika Makutano ya Barabara za Mandela, Morogoro na Sam Nujoma (Ubungo Interchange) unaendelea kwa kasi kubwa na umefikia asilimia 65 kwa mradi mzima na sehemu ya gorofa ya pili ambayo itapitisha magari yanayotumia barabara ya Morogoro imefikia asilimia 75. Mradi huo unatarajiwa kuondoa adha ya msongamano mkubwa katika makutano ya barabara hizo pindi utakapokamilika.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

RC Wangabo Awaonya Wanarukwa Kutokuwa Chanzo cha Mauaji

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mkwamba kilichopo Wilaya ya Nkasi katika ziara yake ya kuelimisha na kuwakataza wananchi kuacha tabia ya kuharibu vyanzo vya maji kwa kufanya shughuli za kibinadamu katika milima ya safu za Lyamba Lyamfipa mkoani Rukwa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewaonya wananchi wanaokaa karibu na milima ya Lyamba Lyamfipa kuacha maramoja kufanya shughuli za kibinaadamu katika milima hiyo baada ya shughuli hizo kuharibu mazingira na vyanzo vya maji vilivyomo na matokeo yake kuwasababishia maisha magumu wananchi wanaoishi katika bonde la ziwa Rukwa lililozungukwa na milima hiyo.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Halmashauri Uvinza Yamkera Naibu Waziri Mabula

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akichomoa moja ya Majalada ya Ardhi katika halmashauri ya Manispaa ya Mpanda jana akiwa katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Katavi.

Na Munir Shemweta –  Uvinza

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt Angeline Mabula ameijia juu Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma kwa kushindwa kuihudumia idara ya ardhi na kusababisha watumishi wa idara hiyo kugharamia baadhi ya vifaa ili kutekeleza majukumu yao.

Hali hiyo ilibainika jana katika halmashauri hiyo wakati Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akiwa katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika Mkoa huo.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Rais Magufuli Awashukuru Mabalozi, Aeleza Mafanikio Makubwa ya Serikali 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewashukuru Mabalozi wanaoziwakilisha nchi mbalimbali hapa nchini kwa ushirikiano mkubwa walioutoa kwa Serikali ya Awamu ya Tano na hivyo kuwa Sehemu ya mafanikio makubwa ya yaliyopatikana nchini Tanzania katika miaka 4 iliyopita.

Mhe. Rais Magufuli ametoa pongezi hizo leo tarehe 21 Januari, 2020 katika hafla ya kuukaribisha Mwaka Mpya aliyowaandalia Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa (Sherry Party) na kufanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail